· *Ni
mtambo wa kwanza kutumiwa na wachimbaji wadogo wa madini Afrika
· *Serikali,
Benki ya Dunia na wamiliki wa migodi mikubwa ya Madini ya Geita na Barrick
washirikiana kuwezesha
Wataalamu wakiunganisha mitambo na wanakijiji katika kijiji cha Lwamgasa wakifuatilia kwa ukaribu shughuli inayofanyika katika kijiji chao huku wakiwa na ndoto za mafanikio.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wakiwa katika eneo lao la kazi wakifanya kazi kwa kutumia dhana duni ikiwemo na madini ya Mercury ambayo ni hatari kwa afya huku wakitarajia kunufaika na mradi na mitambo iliyofikishwa kijijini kwao kwa ukombozi wao.
Mkuu wa Wilaya ya Geita akimkaribisha mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa mradi wa mfano wa uchimbaji mdogo wa madini katika kijiji cha Lwamgasa hivi karibuni.
Naibu Naziri wa Nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Stephen Masele, Mtendaji Mkuu
wa Mgodi wa madini wa Geita Bw. Michael Vananen (kulia), akifuatiwa na Mwenyekiti
wa Kijiji cha Nyamgusu kushoto kwa Mhe. Masele ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Bw.
Omary Mazie Magochie, wakiwa wameshika utepe tayari kwa mgeni rasmi kukata utepe, ikiwa
ni ishara ya uzinduzi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Stephen Masele akifunua kitambaa ili kuweka wazi maelezo ya mradi uliozinduliwa katika eneo la kazi Kijijini Lwamgasa nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Stephen Masele, akiweka mchanga katika mtambo unaozinduliwa ikiwa ni ishara ya kuwa mtambo wanaoletewa wananchi wa kijiji hicho ni mzuri na unafanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Wataalamu wakisafisha mchanga huo ikiwa ni hatua
za awali za kupata dhahabu.
·
SERIKALI kwa kushirikiana
na Benki ya Dunia na wachimbaji wakubwa wa madini nchini imezindua mradi wa
kwanza Afrika wa mfano wa kuchakata dhahabu kwa wachimbaji wadogo wa madini
katika kijiji cha LWAMGASA wilayani Geita.
Mradi huo
umezinduliwa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini)
Mhe. Stephen Masele aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa mradi
huo ulioanza kujadiliwa mwishoni mwa mwaka jana.
Wizara ya Nishati na
Madini kwa kugundua umuhimu na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini katika
uchumi wa nchi ulibuni mradi huu na kuwashirikisha wadau wengine wa maendeleo
wakiwemo Benki ya Dunia, Migodi mikubwa ya dhahabu na Chama cha wachimbaji
wadogo na kusaini mkataba wa makubaliano mnamo mwaka 2009.
Kwa upande wake
mwakilishi toka Benki ya Dunia Mr. Mamadou Barry alizungumzia utekelezaji wa
mradi huo kuwa ni matokeo ya utendaji mzuri wa Serikali ya Tanzania hususan
Wizara ya Nishati na Madini katika kutekeleza miradi inayofadhiliwa na benki
hiyo hivyo kuifanya benki hiyo kuwa na imani na watendaji wake.
Aidha Mamadou
ameeleza kuwa kwa kutambua mchango wa sekta ya madini kwa maendeleo ya Tanzania
na kuwa na nafasi kubwa ya kutoa ajira kwa takribani watanzania milioni moja,
ikiwa ni ajira za moja kwa moja na
zisizo za moja kwa moja, Benki ya Dunia imeona ni vema kuwaendeleza wachimbaji
wadogo ili kuwasaidia katika kukuza uchumi wao binafsi na kuinua kipato cha
taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa wachimbaji wadogo mjini Geita Mr. Christopher Tadeo alizungumzia kuwa uchimbaj mdogo wa madini wilayani Geita ulianza kushamiri
mwaka 1986. Aidha amebainisha changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo katika
uzalishaji wa madini kuwa ni pamoja na uhaba wa mtaji, technolojia duni, elimu
duni, kutokuwa na maeneo ya kutosha kukidhi haja na kiu ya wachimbaji wadogo.
Aidha Bw. Tadeo
ameiomba serikali kutekeleza kwa haraka ahadi walizozitoa kwa wachimbaji wadogo
wa madini ikiwa ni pamoja na kuwanunulia
vifaa kwa ajili ya wachimbaji wadogo, kuwagawia maeneo yanayorudishwa na
wachimbaji wakubwa wa madini, kuwafikishia huduma ya nishati ya umeme katika
maeneo ya machimbo.
Hata hivyo Bw. Tadeo
amethibitisha kuwa mradi uliozinduliwa ni kielelezo tosha cha kutambua mchango
wa serikali hususani uongozi wa wizara kw kutambua uhitaji wa wachimbaji wadogo
wa madini.
Kwa upande wao
wachimbaji wadogo mkoani Geita waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa
pamoja walikiri kuupokea mradi huo kwa mikono miwili na kuishukuru serikali kwa
kuwakumbuka na kutafuta njia za kuwasaidia, aidha walisisitiza umuhimu wa wao
kupatiwa elimu juu ya kuvitumia mitambo hiyo kutokana na ukweli kwamba walizoea
njia duni na kwamba hawana elimu na ujuzi wa kuweza kutumia vifaa hivyo vya
kisasa.
“Sisi hatujasoma sasa
wanasema hiyo mitambo inaendeshwa na wasomi inamaana sisi tutazidi kuwa
masikini”Bi Jenipher Hagai alizungumza kwa huzuni na kuongeza kuwa wanaiomba
serikali ifikilie kuwapa elimu juu ya uendeshaji wa mitambo hiyo jambo ambalo
limekwishakufanyiwa kazi na tayari mpango wa kuwaelimisha wachimbaji hao upo na
kwamba hawatakabidhiwa mitambo hiyo kuiendesha wenyewe mpaka pale watakapopata
mafunzo na kufaulu kutumia vifaa hivyo.
Hayo yalibainishwa na mshauri mwelekezi Bw.John-Bosco Tindebwa
Mkuu wa Wilaya ya
Geita Bw.Omary Magochie aliusifu uongozi wa kijiji cha Lwamgasa kwa utayari
waliokuwa nao baada ya kuoneshwa fursa hii muhimu katika kuinua uchumi wao.
Amebainisha kuwa hatua ya uzinduzi iliyofikiwa ni matunda ya utayari wao.
Ameeleza kwamba awali
mradi huo ulipangwa kutekelezwa katika kijiji cha Nyamgusu ambao waligoma
kuupokea mradi huo kwa sababu zao mbalimbali.
Aidha ameisifu kasi
ya wizara na wadau walioshiriki katika mchakato huu kwa kufanikisha kufikia
hitimisho la mradi huo na kueleza kuwa majadiliano ya uanzishwaji wa mradi
yalianza mwezi oktoba na kabla ya mwaka kwisha tayari matokeo yake
yamekwishapatikana.
Huu ni mwendelezo wa
mipango ya Wizara ya Nishati na Madini katika kuwasaidia wachimbaji wadogo wa
madini, awali wamewawezesha kupata mikopo kupitia Benki ya Uwekezaji (TIB) na
sasa imewawezesha kwa kuwanunulia mtambo wa kuchakata dhahabu ambao utatumika
kama model ya kuendeleza maeneo mengine shughuli za uchimbaji madini
zinakoendelea.
No comments:
Post a Comment