Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mkutano huo.
Msajili wa Bodi hiyo, Jehad A. Jehad akizungumza na wanahabari wakati akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mkutano huo. Kushoto ni Msajili Msaidizi Utawala na Fedha, Angello Ngalla na Msajili wa Bodi hiyo, Jehad A. Jehad.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa (katikati), akiwa na viongozi wenzake wa bodi hiyo. Kutoka kulia ni Kaimu Msajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala, Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad, Msajili Msaidizi Utawala na Fedha, Angello Ngalla na Mwanasheria wa Bodi, Ibrahim Mohamed.
Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkaguzi wa Ndani, Ezekiel Stephen na Kaimu Nsajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Kikao na waandishi wa habari kikiendelea.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi
(AQRB) katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 hadi sasa
imezifungia kampuni 86 kufanyakazi ya ukandarasi baada ya
kushindwa kufuata sheria za ujenzi.
Hayo
yalielezwa na Msajili wa bodi hiyo Jehad Jehad wakati
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
kuhusu mkutano wa usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi
utakaofanyika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
Septemba 18, 2014 jijini Dar es Salaam.
"Kazi
yetu kubwa ni kusimamia sheria ya shughuli za ujenzi na kama tukibaini
kuna kampuni inakwenda kinyume tunaifungia kufanyakazi" alisema Jehad.
Alisema
lengo mkutano huo wa Septemba 18 ni kuwanoa wataalamu wa fani hiyo
ili kukabiliana na mabadiliko ya kiteknologia na kitaaluma katika sekta
ya ujenzi, kubadilishana mawazo na kuboresha huduma za taaluma hiyo.
Akitoa
ufafanuzi wa masuala mbalimbali Mwenyekiti wa bodi hiyo Dk.Ambwene
Mwakyusa alisema Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi
kwa ujumla (Building Codes) itakayoweza kuwabana wajenzi ya maghorofa
ambayo yanabomoka hapa nchini.
Dk. Mwakyusa alisema sheria hiyo ingekuwepo ingewaongoza wataalamu wa
majengo jinsi ya kutumia vifaa vya ujenzi kwenye jengo husika tofauti
na ilivyosasa.
Dk. Mwakyusa
alisema kutokana na sheria hiyo kutokuwepo
wataalamu wa majengo wanapotumia vifaa vya ujenzi
ambavyo havina kiwango na wanapofikishwa kwenye vyombo vya sheria baada
ya majengo wanayojenga kuanguka wanakutwa hawana hatia.
“Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwa
ujumla kama ikiwepo sheria itamuongoza mtaalamu wa majengo afuate sheria iliyopo jinsi ya kutumia
vifaa vya ujenzi mfano kama mbao au nondo zinatakiwa
zitumike aina gani kwenye jengo husika ,”alisema
Dk.Mwakyusa.
Katika mkutano huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Hassan Mwinyi.
No comments:
Post a Comment