Wenyeji Hispania Jumatano hii wanapambana na bingwa wa ulaya Ufaransa na Brazil inakutana na Serbia kwenye mechi zilizosalia za robo fainali ya mashindano ya mpira wa kikapu ya kombe la dunia mjini Madrid, Hispania.
Matumaini ya Serbia kuangusha Brazil ni haba, asema kocha wao Sasha Djordjevic ambaye ameisifu sana timu ya Brazil, akisema ndiyo bora zaidi kwa zote kushiriki mashindano ya kiwango hiki.
Katika mechi ya makundi Brazil ilishinda Serbia 81-73.
Mechi kati ya bingwa wa Ulaya Ufaransa na Hispania itakuwa na kukata na shoka baada Hispania kuibwaga Ufaransa 88-64 mechi za makundi.
Katika mechi za Jumanne usiku za robo-fainali Lithuania, washindi wa shaba mashindano yaliyopita walishinda Uturuki 73-61 na kufuzu kwa nusu fainali ambapo watakutana na bingwa mtetezi Marekani walioichapa Slovenia 119-76.
Mechi za nusu-fainali ni kesho na Ijumaa. Uturuki ilishinda medalio ya fedha m,ashindano yaliyopita nchini Uturuki.
Mashindano haya ya kombe la dunia yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1950 nchini Argentina na wenyeji wakashinda Marekani 60-50 mechi ya fainali.
Kuanzia mwaka wa 1950 hadi 2010 yalijulikana kama mashindano ya ubingwa wa dunia.
Yugoslavia wameshinda mara tano, Marekani wameshinda mara nne na Urusi mara tatu, Brazil mbili na Argentina na Hispania mara moja kila mmoja.
No comments:
Post a Comment