TANGAZO


Saturday, September 27, 2014

Kinana afanya kweli Jimbo la Korogwe Vijijini kwa Profesa Maji Marefu


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwapungia wananchi walipowalisi kwenye mkutano wa hadhara, Mombo, Korogwe Vijijini. (Picha zote na Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio Blog)

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara, mjini Mopmbo, Korogwe Vijijini
Katibu Mkuu akipiga makofi baada ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo la CCM Kata ya Masewa, Korogwe Vijijini, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa  Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani wakishiriki ujenzi wa jengo hilo la CCM Kata Mashewa, Jimbo la Korogwe Vijijini.
Kinana akishiriki katika ujenzi wa jengo la Maabara katika Shule ya Sekondari ya Mashewa, Korogwe Vijijini.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu wa jina la Profesa Maji Marefu akimueleza Kinana kuhusu matatizo ya kutokwepo minara ya mawasiliano katika baadhi ya vijiji jimboni humo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Buna,Korogwe Vijijini
Kinana  akishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Buna,Korogwe Vijijini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishona upindo wa khanga katika Kituo cha Ushonaji cha Wajasiriamali  mjini Mombo, katika Jimbo la Korogwe Vijijini, Mkoa wa Pwani jana, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. Kulia ni Mkufunzi wa chuo hicho, Veronica Simba pamoja na wanafunzi wa chuo hicho.
Kinana na viongozi wengine wa CCM wakipita katika moja ya mitaa ya Mji wa Mombo, Korogwe Vijijini.
Vijana wa CCM wakishangilia wakati Kinana akiingia kwenye mkutano wa hadhara mjini Mombo, Korogwe Vijijini.
 Kinana akiwasalimia wananchi katika mkutano huo.
Kikundi cha sanaa kikitumbuiza wakati wa mkutano huo wa hadhara.
  Msanii akisikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo.
Kinana akiagana na wananchi baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Kinana akiagana na kiongozi wa jamii ya kimasai baada ya kumalizika mkutano huo.
Kinana akishukuru baada ya kukabidhiwa zawadi na jamii ya kimasai katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment