Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Samia Suluhu Hassan, akiongeza mjadala toka kamati mbalimbali za Bunge hilo leo
9 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Juu na chini: Baadhi wa Wajumbe wa Kamati mbalimbali za Bunge Maalum la Katiba wakichangia mada katika mjadala Bungeni hapo leo 9 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Juu na chini: Baadhi wa Wajumbe wa Kamati mbalimbali za Bunge Maalum la Katiba wakichangia mada katika mjadala Bungeni hapo leo 9 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Juu na chini: Baadhi wa Wajumbe wa Kamati mbalimbali za Bunge Maalum la Katiba wakichangia mada katika mjadala Bungeni hapo leo 9 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Samia Suluhu Hassan, akifuatilia mjadala toka kamati mbalimbali za Bunge hilo
leo 9 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Samia Suluhu Hassan, akifuatilia mjadala toka kamati mbalimbali za Bunge hilo
leo 9 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Samia Suluhu Hassan, akifuatilia mjadala toka kamati mbalimbali za Bunge hilo
leo 9 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Baadhi ya madereva wa Treni ya TAZARA walipata wasaa
wa kuhudhuria mjadala huo Bunge Maalum la Katiba hivi leo 9 Septemba, 2014
mjini Dodoma.
Bungeni hap oleo 9 Septemba, 2014.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
wakifuatilia mjadala ukioendelea
Bungeni hap oleo 9 Septemba, 2014.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
wakifuatilia mjadala ukioendelea
Waziri wa Katiba na Sheria, Asha Rose Migiro, akitetea jambo na Naibu wake, Anjela kairukhuwakatiWajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Edward Lowassa na Williuam Lukuvi wakiteta jambo wakati wa kikao cha bunge hilo jana.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na kuhudhuria mjadala ukioendelea Bungeni hap oleo 9 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Wanafunzi 17 kutoka Kondoa Centre of Technology nao ni moja ya wageni waliopata wasaa wa kutembelea Bunge Maalum la Katiba na kuhudhuria mjadala ukioendelea Bungeni hap oleo 9 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Bunge Maalum la Katiba
laanza mijadala ya Rasimu ya Katiba rasmi leo.
Na Benedict Liwenga,
Maelezo-Dodoma.
BUNGE Maalum la Katiba leo tarehe 9 Septemba, 2014 limeanza
kazi yake ya kusoma na kujadili taarifa za Kamati mbalimbali zikiwemo Kamati
namba Kumi na Mbili, Kamati namba Mbili, Kamati namba Moja, Kamati namba Nne,
Kamati namba Nane, Kamati namba Tano, Kamati namba Tisa, Kamati namba Tatu,
Kamati namba Sita pamoja na Kamati namba Kumi na Moja.
Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika Bunge hilo ni pamoja
suala la baadhi ya viongozi kumiliki akaunti zao za fedha nje ya nchi, haki za
makundi mbalimbali nchini, haki za binadamu, masuala ya ndoa ya jinsia moja,
haki za wafanyakazi na ajira, wajibu wa Waajiri nchini, haki za uzazi kwa
wanawake, haki ya kuishi na sheria ya kunyonga, pia mambo yanayohusu Muundo wa
Baraza la Usalama la Taifa.
Akizungumza wakati wa mjadala huo katika Bunge hilo, mjumbe
wa Kamati namba Sita, Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa si vema kwa viongozi
nchini kujenga tabia ya kufungua akaunti na kuweka fedha zao nje ya nchi kwani
kunakaribisha masuala ya wizi wa fedha toka ndani ya nchi kwenda nje ya nchi.
“Ni vema kiongozi yoyote anayetaka kumiliki fedha nje ya nchi
aeleze ni wapi anamiliki hizo akaunti na nini anamiliki”, alisema Mhe. Mwijage.
Naye Mjumbe wa Kamati namba Tatu, Mhe. Nyambari Chacha
Nyangwine amegusia kuhusiana na suala hilo akisema kuwa kuna haja ya kuwekwa
kwa sheria itakayowabana viongozi wenye tabia ya kufungua akaunti za fedha nje
ya nchi ili hali hiyo isiwepo nchini.
“Mambo ya kiongozi wa umma kumiliki akaunti ya fedha nje ya
nchi si jambo jema, sheria izuie na ni vema kiongozi yoyote wa umma anayetaka
kufanya hivyo basi afungue akaunti yake ndani ya nchi na sio vinginevyo”,
alisema Nyangwine.
Mhe. Nyangwine pia amezungumzia kuhusu kuendelezwa kwa sekta
ya viwanda nchini ili kuweza kujikwamua kiuchumi, hivyo ameisisitizia Serikali
kuviendeleza viwanda vyake ili uchumi wa nchi uweze kukua na kuleta maendeleo
kwa wananchi.
Aidha, alliongeza kuhusu haki za wanaume huku akisema kuwa
wanaume tayari wao wanazo haki zao tangu kuzaliwa kulingana na maandiko ya dini
yanavyosema, hivyo ni vema sasa wanawake wakapewa kipaumbele kwa kupewa haki
sawa yaani hamsini kwa hamsini.
Katika hali nyingine, mjumbe mwingine Mhe. Amon Mpanju amezungumzia
kuhusu ripoti ya kamati yake iliyogusia masuala ya haki za makundi mbalimbali
yakiwemo, vijana, wazee pamoja na Watu wenye ulemavu nchini.
Mhe. Mpanju ameeleza kuwa Ibara ya 45 imekazia kuhusu haki za
watu wenye ulemavu waweze kushiriki katika vyombo vya uwakilishi, hivyo yeye
pamoja kamati yake wameshauri kuwepo na kipaumbele kwa watu hao ikiwemo
miundombinu iliyorafiki kwa watu wa namna hiyo izingatiwe ili waweze kufanya
majukumu yao kama wengine, lakini ameshauri kuzipa kipaumbele haki za makundi
mengine wakiwemo vijana na wazee.
Kuhusiana na suala la ndoa za jinsia moja, mjumbe wa kamati
namba Kumi na Moja Mhe. Adeligunda Mgaya amesema kuwa katika Sura ya Nne inayohusiana
na haki za binadamu pamoja na Ibara ya 28 ya haki ya falagha na haki ya mtu,
yeye pamoja na kamati yake wameshauri kuwa ndoa za jinsia moja zisitambuliwe na
ameshauri juu ya kuwepo kwa kifungu ambacho kitatoa katazo la marufuku kwa
Tanzania kuwa na ndoa za namna hiyo.
Mhe. Mgaya ameongeza kuwa katika Ibara ya 36 ya Sura ya Nne
inayohusiana na mambo ya haki za wafanyakazi na ajira, amesema kuwa wafanyakazi
wengi wanakosa haki ya uwakilishi wa vyombo vya maamuzi hivyo ameshauri kuwepo kwa
vyomnbo hivyo ili wafanyakazi wapate kuwa na uwakilishi katika maamuzi.
“Ushiriki wa vyombo vyenye maamuzi sio mzuri ndiyo maana kuna
migogoro mingi licha ya kuwepo na Mabaraza ya wafanya kazi ambayo yamekuwa
yakisisitiza kuhusu hilo lakini bado migogoro ipo”, alisema Mhe. Mgaya.
Aidha, Mhe. Mgaya amesisitiza juu ya Waajiri nchini kutambua
wajibu wao kama ilivyo kwa waajiriwa lakini akagusia suala la kutoa kipaumbele
katika suala la uzazi salama kwa wanawake ili waweze kupatiwa huduma bure ya
uzazi na akashauri juu ya suala la ardhi katika Katiba mpya ijayo lisiwe suala
la Muungano.
No comments:
Post a Comment