Shirika la afya duniani WHO
limeonya kuwa ueneeaji wa haraka wa Ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa
Afrika si jambo la kawaida na kwamba itachukua miezi kadhaa ili
kuudhibiti ugonjwa huo.
limeonya kuwa viwango vya ugonjwa huo vilipuuzwa kwa sababu nyingi ikiwemo ile ya familia kuwaficha wagonjwa katika majumba yao.Shirika hilo pia limesema kuwa kuna maeneo ambayo maafisa wa matibabu hawawezi kufika.
Kufikia sasa zaidi ya vifo 1400 vimethibitishwa nchini Liberia,Guinea,Sierra leone na Nigeria.
No comments:
Post a Comment