Watu watano waumini wa dhehebu
lililopigwa marufuku nchini Uchina wamefikishwa mahakamani kujibu
mashtaka ya kumpiga mwanamke mmoja hadi akafa.
Watano hao wafuasi wa dhehebu la ''Church of
Almighty God'' walimvamia mama huyo katika mkahawa wa McDonalds katika
mji wa Shandong ulioko mashariki mwa China.Mama huyo Wu Shuoyan - alipigwa mbele ya mwanawe mwenye umri wa miaka 7 baada ya wafuasi wa dhehebu hilo kudai alikataa kupeana nambari yake ya simu ya mkononi kwa mmoja wa washiriki wa dini hiyo ambaye alitaka kumshawishi kujiunga na dini hiyo.
Mauaji ya Wu yaliwatamausha wachina ambao hawakuamini kuwa watu wangeweza kutekeleza mauaji mbele ya Umma.
Wateja wa McDonalds walioshuhudia tukio hilo walidai kuwa walionywa wasiingilie kamwe tukio hilo la sivyo wembe utakuwa ni huohuo.
Dhehebu hilo linazaidi ya wafuasi milioni moja nchini humo licha ya kuwa limepigwa marufuku .
Mafundisho ya dhehebu hilo yanadai kuwa yesu Kristo alifufuka katika maumbili ya mwanamke wa Kichina.
Mamia ya wafuasi wa dhehebu hilo wamekamatwa nchini Uchina tangu mauaji ya Wu mwezi Mei.
No comments:
Post a Comment