Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa
wa kundi la Al Qaeda kusini mashariki mwa Yemen wamewateka na kuwaua
takriban wanajeshi 14 waliokuwa wakirudi nyumbani kutoka kazini
mashariki mwa taifa hilo.
Wanajeshi hao walidaiwa kuwa katika likizo wakati basi lao liliposhambuliwa na wanamgambo hao kabla ya kutekwa nyara.Maafisa katika eneo hilo wanasema kuwa walipata miili yao saa chache baadaye karibu na mji wa Sieyoun katika mkoa wa Hadramout.
Kumekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wanajeshi wa serikali ya Yemen yanayotekelezwa na wanamgambo wa kundi la Al Qaeda.
No comments:
Post a Comment