Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akizungumza na baadhi viongozi na wajumbe kutoka Chama cha Wakulima Wadogo wadogo wa zao la Pamba Tanzania (TACOGA) katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.
Kaimu Mwenyekiti wa kutoka Chama cha Wakulima Wadogo wadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA), Godfrey Mokiri(katikati) akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta(kulia) katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo wakati baadhi viongozi na wajumbe wa chama hicho walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.Kushoto ni Katibu wa chama hicho, George Mpanduji.
Baadhi viongozi na wajumbe wa Chama cha Wakulima Wadogo wadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (wanne kushoto) na Katibu wa Bunge hilo, Yahaya Khamis Hamad (wa tatu kulia )walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.
Na Magreth Kinabo, DODOMA
Chama cha
Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) kimemwomba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe . Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete
asisitishe mchakato wa mijadala
ya Bunge Maalum la Katiba , kwani kitendo cha kusitisha ni kuzuia makusanyo ya mawazo mtambuka ya wabunge .
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu chama hicho,
George Mpanduji wakati
akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta Maalum ofisini kwake mjini Dodoma leo kwa
lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa
kuomba Bunge Maalum la Katiba
kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa
mahitaji ya wakulima Tanzania.
Mpanduji aliambatana na baadhi wa viongozi na wajumbe kutoka
mikoa 11 wa TACOGA ,alisema wanaheshimu makubaliano ya kisiasa ya kutungwa
Katiba ya Nchi, lakini tunatahadharisha kuwa shurti za kisiasa zinazopiganiwa
na vyama vya upinzani Bungeni hadi kuzuia wabunge kutetea haki mtambuka za
kijamii suala hilo linaleta hitilafu ya kuchelewesha mahitaji muhimu kama ya
kujengwa amani kati ya wakulima na wafugaji.
“ Vikao vya
Bunge Maalum viendelee na wabunge
wote watangulize kwanza maslahi ya umma dhidi ya misukumo batili iliyo
kinyume na maslahi mapana ya umma na taifa.
Wabunge hawa wanafikra chanya za
kujenga makutano ya fikra patanifu ya kupatikana suluhu za haki za makundi
mbalimbali, hususani pale palipo na ombwe la matakwa hayo Katika ya sasa,”
alisema Mokiri.
Aidha
Mpanduji aliongeza kwamba wanashauri agenda za haki mbalimbali kwa jamii zipewe
vipaumbele kwa kuwa pana vilio vya kuhitajika suluhu za haraka kwa
mahitaji mbalimbali ya makundi ya umma.
Mpanduji
alisema wakulima hao, wanataka Katiba ipatiokane haraka kwani itakuwa
suluhisho dhidi ya mizozo na maafa yanayotokea nchni kati ya wakulima na
wafugaji.
“ Tunahimiza
vyama vya siasa vishindanishe hoja za kukonga mioyo kwa kutetea haki za jamii
na taifa dhidi ya kutambulisha misukumo y shurti za utashi wa makundi ya watu
ya maslahi binafsi,” alisisitiza.
Alisema chama
hicho ,pia kinampongeza Mhe. Sitta kwa uvumilivu wake na hekima ya uongozi na
wabunge wote wanaohudhuria vikao vya Bunge hilo kwa kuwa wanatimiza uzalendo
wao, uaminifu wao na utiifu wao wa kutumikia jamii na taifa.
Chama hicho
kimtaka mlezi wao ambaye ni John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Maghribi,
ambaye waliochagua kuanzia mwaka 2012 kuendelea kuhudhuria vikao vyote vya Bunge hilo ili
akasimamie maslahi yao na aungane na vikundi vinavyoandaa na kutetea haki za
wakulima Tanzania.
Kwa upande
wake Mhe. Sitta alisema lengo la kutungahiyo ni iwe rafiki yenye
kukidhi matakwa ya wananchi.
Miongoni mwa
hoja nyingine walizozungumzia ili Katiba itamke ni haki ya mikopo kwa wakulima,
ruzuku wa wakulima, iwalinde na itamke haki za wanawake katika kumiliki ardhi
wanapofiwa na waume zao na kufadika na mapato ya kilimo.
No comments:
Post a Comment