TANGAZO


Wednesday, August 27, 2014

Viongozi na wasanii wa vyama vya mashirikisho ya sanaa wasisitiza kuhusu ujio wa ujumbe wao Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET) Bw. John Kitime (kushoto) akiwahutubia waandishi wa Habari pamoja na Wasanii waliohudhuria mkutano uliofanyika mjini Dodoma 27 Agosti, 2014. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifwamba.
Mwakilishi wa Wasanii kutoka Zanzibar, Bw. Makame Juma (kushoto) akisisitiza jambo kuhusu ujio wa Ujumbe wao Bunge Maalum la Katiba wakati wa mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika mjini Dodoma 27 Agosti, 2014. Kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET) Bw. John Kitime. 
 Baadhi ya wasanii mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini maelezo toka kwa viongozi wao wakati wa mkutano uliofanyika mjini Dodoma 27 Agosti, 2014.
 Baadhi ya wasanii mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini maelezo toka kwa viongozi wao wakati wa mkutano uliofanyika mjini Dodoma 27 Agosti, 2014.
 Baadhi ya wasanii mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini maelezo toka kwa viongozi wao wakati wa mkutano uliofanyika mjini Dodoma 27 Agosti, 2014.
Baadhi ya wasanii mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini maelezo toka kwa viongozi wao wakati wa mkutano uliofanyika mjini Dodoma 27 Agosti, 2014. 
Baadhi ya waandishi wa Habari wakitekeleza majukumu yao wakati wa mkutano na Shirikisho la Wasanii uliofanyika mjini Dodoma 27 Agosti, 2014. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)


Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma
27/08/2014.
VIONGOZI na Wasanii toka baadhi ya Vyama na Mashirikisho ya Sanaa nchini wameendelea kuhabarisha umma juu ya ujio wa Ujumbe wao wenye malengo mawili ya msingi ya kutaka wasanii kutambuliwa kama kundi kubwa maalum pamoja na milikibunifu (Intellectual property).

Msisitizo huo umetolewa leo 27 Agosti, 2014 na mmoja wa wawakilishi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET) Bw. John Kitime wakati walipofanya mkutano na waandishi wa Habari leo katika Hoteli ya Dodoma mjini humo.

Bw. Kitime ameeleza kuwa walikuja Bungeni mjini Dodoma na mapendekezo ya namna ya kuingiza hoja zao ambazo zilisahauliwa na sio Ibara Mpya kama baadhi ya vyombo vya Habari vilivyoandika.

Kitime ameongeza kuwa mapendekezo yao ni kuwa katika Ibara ya 30 iongezwe Aya moja tu, na Ibara ya 37 ambayo ionaongelea juu ya haki ya ulinzi wa mali itambue kuwa pamoja na mali zinazohamishika, pia kuna mali isiyoshikika.

“Tumepata faraja kubwa kupokelewa na Bunge hili Maalum la Katiba na kuweza kuzunguka kwenye Kamati 9 kwa siku hizi mbili na kukumbushia mapendekezo yetu haya ambayo hayabebi tu wasanii, bali pia Wavumbuzi wa kiteknolojia, wasomi watafiti na wananchi wote kwa ujumla”. Alisema Kitime.

Akizungumzia kuhusu maombi yao makubwa mawili yaliyowaleta tokea awali, Bw. Kitime amefafanua kuwa wanahitaji wasanii wapate kutambuliwa kama kundi maalum kama yalivyotambuliwa makundi mengine ya wakulima, wafugaji na wavuvi, na Pili ni kuhusiana na suala la Milikibunifu (Intellectual Property) ikiwa kama moja ya aina za mali zinazohitaji kulindwa katika Katiba.

Naye Kiongozi wa msafara wa wasanii hao ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) amesisitiza juu ya umuhimu wa Katiba Mpya itakayopatikana iwakumbuke wasanii kwani wao kama wao wana haki ya kikatiba na hivyo wanahitaji ulinzi wa mali zao zisizoshikika (Intellectual property).

“Katiba ni ya Watanzania wote, kila mtanzania ana haki yake ya kimsingi kikatiba na hivyo hizi hoja zetu tulizoziwasilisha kama wasanii wa Tanzania ni za msingi”. Alisema Mwakifwamba.


Hii ni mara ya Tatu kwa kundi hili la wasanii wakiwemo viongozi wao kukutana na Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba ambapo mchakato uliowafikisha ulianza kwa Mashirikisho kukutana na kutengeneza Baraza la Katiba ambapo Mashirikisho yalitoa mapendekezo kadhaa yaliyofikishwa kwenye Tume ya Katiba.

No comments:

Post a Comment