TANGAZO


Tuesday, August 12, 2014

Tanzania yaandaa mkutano wa Magavana

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 30 wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki (BOG) utakaofanyikia jijini Dar es salaam tarehe 22 mwezi huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile na Rais wa Benki ya PTA kwa vyombo vya habari, mkutano huo utakuwa wa siku moja.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa lengo la mkutano huo ni  kujadili masuala mbalimbali ya kibenki ikiwemo mpango mkakati wa benki hizo na masuala ya fedha na uchumi kwa nchi washirika.

Wajumbe wa mkutano huo ni Mawaziri wa Fedha na uchumi wa nchi washirika ambao ndio chombo cha juu cha ngazi ya maamuzi ya benki katika nchi zao.

Aidha, taarifa hiyo imeongeza  kuwa mkutano huo utatanguliwa na semina ya wafanyabiashara itakayofanyika Agosti 21 siku moja kabla ya mkutano mkuu wa Magavana hao.

Benki ya PTA ilianzishwa mwaka 1985 ikiwa na jumla ya washirika 22 ikiwemo nchi 18 ambazo ni Burundi, Comoros, Djibouti na Congo.

Nchi nyinine ni Misri, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Malawi, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Somalia, Sudan, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.

Aidha, PTA inashirikiana na nchi nyingine nje ya bara la Afrika ambazo ni Belarus na China.
Washirika wengine Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Kampuni ya Bima ya Mauritia iitwayo Eagle na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Mauritius.

No comments:

Post a Comment