Rais wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina akimshikilia shingo Master Hudu Thabit akionesha moja ya mbinu inazotumika kwa kujihami kwa ajili ya usalama.
Rais wa UPAM duniani Prof. Maurizi
Mardina (kushoto) baada ya kuonesha mbinu ya kujihami kwa mwandishi wa habari
Kibwana Dachi (aliyekaa). Kulia ni Master Hudu Thabit. (Picha zote na Eleuteri
Mangi-MAELEZO)
Na Rose Masaka-MAELEZO
11/08/2014
UMOJA wa Wapiganaji wa Sanaa
ya Mapigano Duniani (UPAM) unaandaa shindano la kimataifa la wapiganaji ambalo
linatarajiwa kufanyika nchini kati ya Mwezi Desemba mwaka huu na mwanzoni mwa
mwaka ujao kutokana na ruhusa itakayotolewa na Serikali kwa mamlaka
zinazohusika.
Kauli hiyo imetolewa leo
na Rais wa UPAM Prof. Maurizi Mardina alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam
Profesa Mardina amesema
kuwa mchezo wa kupigana ni mchezo mzuri ambao unahitaji kujitoa na uwezo mzuri
wa kufikiri na siyo mchezo au mafunzo yanayosababisha uonevu bali ni mafunzo
yanayompa mtu uwezo wa kujilinda na kujitetea.
Ameongeza kwa kusema
kuwa Nchi 102 zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watashiriki wachezaji
25 wa umri na jinsia zote kutoka katika nchi hizo.
“Walimu wanafundisha
vizuri ili kuandaa timu bora na baadhi ya vifaa tayari vimenunulia vyenye
thamani ya dola ya kimarekani 25000.” amesema Mardina.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
wa UPAM Tanzania Joe Jolamu ameeleza kuwa mashindano ya ndani tayari
yameishaanza na yanaendelea ili kuweza kupata timu moja ya taifa itayocheza
katika mashindano ya dunia.
“Wachezaji ambao
wataruhusiwa kujiunga na kuingia katika kuchezea timu ya dunia ni wale tu ambao
wapo katika kikosi maalumu” alisema mwalimu Jolamu.
Aidha, mmoja wa
wanafunzi wa mchezo huo Hafidhi Kunambi anayepata mafunzo ya mchezo huo
ameonesha jinsi alivyojifunza namna ya kujilinda kadiri ya mafunzo aliyopata.
Kwa Tanzania wanatakiwa
washiriki 45 ambao wamefanya mazoezi ili kuweza kushiriki mashindano hayo
kutoka maeneo mbalimbali nchini na kupata timu bora itakayoleta ushindi.
No comments:
Post a Comment