TANGAZO


Saturday, August 2, 2014

Serikali ya Tanzania yakanusha tuhuma za kuwatelekeza wanafunzi na raia wake nchini Ukrain

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, alipokuwa akikanusha madi ya kutelekezwa kwa wanafunzi wa Tanzania, waliopo nchini Ukreain Mashariki kulikotangazwa na kituo cha nje cha habari hivi karibuni. Kushoto ni Ofisa Habari wa wizara hiyo, Ally Kondo. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Na Magendela Hamisi
SERIKALI ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu ya madai ya kuwatelekeza Watanzania wanaoishi na kusoma nchini Ukraine ambayo kuna machafuko.

Siku chache zilizopita moja ya chombo cha habari cha Kimatifa, kilidaiwa kutangaza kuwa Serikali ya Tanzania inalalamikiwa na baadhi ya wanafunzi walioko nchini Ukraine kwa madai ya kushindwa kuwapa msaada licha ya kuwepo hali ya machafuko nchini humo.
Madai hayo yalidaiwa kutolewa na mmoja wa wanaodaiwa kuwa ni Mtanzania, mwanafunzi aliyefahamika kuwa anayesoma nchini humo, ambaye alifahamika kwa jina moja tu la Shamila.

Pia ilidaiwa kuwa shirika hilo, la habari la kimataifa, lilidaiwa kufanya mahojiano na baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao, waliopo Zanzibar nao, waliodaiwa kukiri kuwepo kwa hali hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally leo jijini Dar es Salaam, alitoa ufafanuzi na kukanusha taarifa hizo, kuwa si za kweli, ambazo zilidai pia kwamba Serikali haikuwajali na iliwatelekeza wanafunzi wanaosoma nchini humo ambako kuna machafuko.
"Wizara imesikitishwa na taarifa hiyo iliyotolewa na BBC bila kufanyiwa uchunguzi wa kina, ukweli ni kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi amnao pia unawakilisha Ukraine, ulichukua hatua za haraka kuwandoa wanafunzi wote ili kuwa salama.

"Ubalozi ulishirikiana na Rais wa wanafunzi wa Tanzania katika mji wa Lugansk, Ahmad Juma na walifanikiwa kuwaondoa watanzania wote 32 katika mji huo ulioko vitani na kuwapeleka katika mji wa Kharkov ambako ni shwari," alisema

 Alifafanua kuwa Serikali kupitia ubalozi wake Moscow uliwaombea wanafunzi hao malazi kwenye Chuo cha Kharkov Technical University, ambao walikubali kutoa hosteli ingawa wanafunzi wengi walimua kurudi nyumbani isipokuwa wanafunzi saba pekee.
Aliongeza kuwa kati ya wanafunzi hao 20 walidhaminiwa na Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar kupitia Bodi ya Mikopo, pia aliongeza kuwa orodha ya wanafunzi walikuwa nchini Ukraine haijumishi jina la Shamila ambaye ilidaiwa alihojiwa na BBC.

Baada ya uchunguzi wa kina ilibainika kuwa Shamila alishamaliza kusoma nchini humo na sasa anajishughulisha na udalali wa wanafunzi wanaohitaji kusoma nchini humo.

"Habari hiyo iliyoandikwa ilikuwa ya upande mmoja bila kuulizwa Serikali hali ambayo haikukidhi vigezo pia ni ya kizindaki na uongo mtupu," alisema.

No comments:

Post a Comment