Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma akitoa hotuba yake fupi mbele ya
wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Jiolojia uliofanyika katika Ukumbi wa
Kimataifa wa J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa, Sospeter Muhongo akitoa hotuba yake mbele ya
wajumbe (hawako pichani) baadhi ya kazi mbalimbali alizowahi kuzifanya katika
maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi pamoja na mada Kuu ya Mkutano wa
Jiolojia uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa
J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamini Wiliam Mkapa
akiwahutubia wajumbe waliohudhuria mkutano wa Jiolojia uliofanyika katika
Ukumbi wa Kimataifa wa J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Baadhi wa wajumbe waliohudhuria mkutano wa Jiolojia
wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi katika Ukumbi
wa Kimataifa wa J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Baadhi wa wajumbe waliohudhuria mkutano wa Jiolojia
wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi katika Ukumbi
wa Kimataifa wa J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamini Wiliam Mkapa
(wa pili toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria
mkutano wa Jiolojia uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa J.K Nyerere
Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa
Abdulkarim Mruma, anayemfuatia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini,
Mhe. Stephen Masele. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa
Sospeter Muhongo. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo)
Na Benedict Liwenga-MAELEZO
RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini William
Mkapa amezitaka jamii nyingi za kiafrika kuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na
mchango wa sayansi na teknolojia katika kuleta maendeleo nchini.
Mhe. Mkapa ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua
mkutano wa Jiolojia uliowakutanisha wataalam mbalimbali wa mambo ya jiolojia
ulimwenguni akiwa ameongozana na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa
Sospeter Muhongo pamoja na Naibu Waziri wake, Mhe. Stephen Masele.
Mhe. Mkapa ameeleza kuwa ni vema kwa wanasayansi
ulimwenguni kujenga utamaduni wa kukutana mara kwa mara na kujadili mambo yanayohusu
sayansi na teknolojia ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii
ambazo zitatatua migogoro inayoweza kujitokeza baina ya nchi na wawekezaji.
“Jamii nyingi za kiafrika hazijaelewa mchango mkubwa
wa sayansi na teknolojia katika kuleta maendeleo lakini maendeleo daima
yanatokana na rasilimaliwatu juu ya ardhi na chini ya ardhi, mchango wake huu
hauthaminiwi na wengi lakini wanaoweza
kufanya hivi ni wanasayansi”. Alisema Mhe. Mkapa.
Aidha, Mhe. Mkapa ameishauri serikali licha ya kudhamini
mafunzo mbalimbali na masomo kwa vijana nje na ndani ya nchi, fedha za kutosha
bado zinahitajika katika kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakuwa endelevu.

No comments:
Post a Comment