TANGAZO


Thursday, August 14, 2014

Rais Kikwete alifungua Kongamano la Kwanza la Diaspora wa Tanzania jijini Dar es Salaam

Rais Jakaya Kikwete, akipatiwa maelezo na Meneja Masoko wa Kampuni ya Simu ya Huawei, Lydia Wangari (kulia), alipotembele banda la kampuni hiyo wakati alipofungua Kongamano la Kwanza la Watanzania wanaoishi nchi mbalimbali za nje (Diaspora), jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Rais Jakaya Kikwete, akiangalia moja ya simu za Kampuni ya Huawei, alipotembelea banda la kampuni hiyo wakatiwa kongamano hilo leo. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na anayempatia maelezo ni Meneja Masoko wa kampuni hiyoi, Lydia Wangari.
Rais Jakaya Kikwete, akipatiwa maelezo na Mkurgenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tan Trade), Jacqqqueline Maleoko (wa pili kushoto), alipotembele banda la mamlaka hiyo wakati alipofungua Kongamano la Kwanza la Watanzania wanaoishi nchi mbalimbali za nje (Diaspora), jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akipatiwa maelezo na Mkurgenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kushoto), alipotembele banda la mfuko huo, wakati wa kongamano hilo, jijini leo. Wapili kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa mfuko huo, Lulu Mengele. 
Rais Jakaya Kikwete, akipatiwa maelezo na Mkurgenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (wapili kushoto), alipotembele banda la mfuko huo, jijini leo. Watatu kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa mfuko huo, Lulu Mengele. 
Rais Jakaya Kikwete, akipatiwa maelezo na Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba laTaifa (NHC), Tuntufye Mwambusi, alipotembele banda la shirika hilo, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo. 
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akipatiwa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba laTaifa (NHC), Nehemia Mchechu (wapili kulia), alipotembele banda la shirika hilo, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo. 
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akielezea jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba laTaifa (NHC), Nehemia Mchechu (kulia), alipotembele banda la shirika hilo, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba laTaifa (NHC), Nehemia Mchechu (kulia), alipotembele banda la shirika hilo.
Rais Jakaya Kikwete, akiingia kwenye ukumbi wa mikutano Hoteli ya Serena, kwa ajili ya kulifungua Kongamano la Kwanza la Diaspora jijini leo.
Baadhi ya Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora), wakipiga makofi kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete kulifungua kongamano lao la kwanza nchini.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa Diaspora, alipofika Hoteli ya Serena jijini kulifungua kongamano hilo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika meza kuu wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo. 
Rais Kikwete akiwa na Mkurugenzi wa DIASPORA Tanzania, Emmanuel Mwachullah (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Wahamizi (IOM), Damien Thuriaux (kushoto), wakiimba wimbo wa Taifa.
Baadhi ya wanadiaspora wakiimba wimbo wa Taifa katika kongamano hilo.
Baadhi ya wanadiaspora wakiimba wimbo wa Taifa katika kongamano hilo.
Rais Kikwete akiwa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) na Mkurugenzi wa DIASPORA Tanzania, Emmanuel Mwachullah (kushoto), wakiimba wimbo wa Taifa.
Rais Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia), wakiimba wimbo wa Taifa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rosemary Jairo (kulia) katika kongamano hilo.
Mkurugenzi wa DIASPORA Tanzania, Emmanuel Mwachullah, akitoa neno la utanguliza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo jijini leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rosemary Jairo, akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza wakati wa kongamano hilo, kabla ya kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete kulifungua kongamano hilo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza wakati wa kongamano hilo, kabla ya kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete kulifungua kongamano hilo.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akilifungua kongamano hilo, Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo.


Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akilifungua kongamano hilo, Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akilifungua kongamano hilo, Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati akilifungua kongamano hilo, Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanadiaspora wa Tanzania wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete, alipokuwa akizungumza wakati akilifungua kongamano hilo, Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo.  
Baadhi ya wanadiaspora wa Tanzania wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete, alipokuwa akizungumza wakati akilifungua kongamano hilo, Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo. 
Mwandishi wa habari wa ITV, Jackline Silemi, akiwa kazini wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati akilifungua kongamano hilo, jijini leo.
Rais Jakaya Kikwete, akisisitiza jambo, alipokuwa akizungumza wakati akilifungua kongamano hilo, Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akifafanua jambo, alipokuwa akizungumza wakati akilifungua kongamano hilo, Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akibonyeza kitufe cha kompyuta alipokuwa akizindua mtandao wa Tanzania Diaspora, wa www.tandispora.org, wakati alipokuwa akilifungua Kongamano hilo, la The First Diaspora Homecoming, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati), Mkurugenzi wa DIASPORA Tanzania, Emmanuel Mwachullah (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Wahamizi (IOM), Damien Thuriaux (wapili kushoto), wakipiga makofa mara baada ya Rais kuuzindua mtandao huo wa Wanadispora wa Tanzania wa www.tandispora.org, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akitetea jambo na Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Leticia Nyerere (kushoto), wakati alipolizindua kongamano hilo. Wapili kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akipiga picha ya kumbukumbu na Kamati ya maandalizi ya kongamano hilo, mara baada ya kulifungua leo. Kushoto kwake ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akipiga picha ya kumbukumbu na moja ya makundi ya wanadispora hao wa Tanzania, mara baada ya kulifungua kongamano lao leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya viongozi wa wanadispora hao wa Tanzania pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi wadau wa Diaspora, mara baada ya kulifungua kongamano hilo, leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na mmoja wa wanadispora wa Tanzania, mara baada yakumalizika shughuli za kupiga picha za kumbukumbu za tukio hilo la uzinduzi wa Kongamano lao leo, jijini Dar es Salaam. 

Na Kassim Mbarouk
RAIS Jakaya Kitwete ametoa wito kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi DIASPORA kukumbumba kuwekeza nchini.
Kikwete aliyasema hayo leo, wakati akizindua kongamano la kwanza la DIASPORA la The First Diaspora Homecoming, lililofanyika jijini Dar es Salaam.

"Nilazima mkumbuke nyumbani muwekeze na kuleta wawekezaji nchini  kwa maendeleo ya nchi yenu Tanzania ni nchi yenu hivyo kuwa nje ya nchi isiwe sababu ya kushindwa kuwekeza" alisema Kikwete.

Kama hiyo haitoshi pia Kikwete amewasisitiza  Watanzania hao kuweka akiba katika benki za hapa nyumbani ambazo hivi sasa zimefungua fursa hizo  kwa DIASPORA.

Aidha Kikwete aliongeza kwa kuwaambia DIASPORA waachane na imani potofu  ya kuwa huku ni kubaya kwa sababu nyumbani ni nyumbani, hivyo umuhimu wa kuwekeza  nyumbani upo.

Kaeni ugenini lakini kumbukeni nyumbani pia nyoye mnapaswa kufikiria mtarudi vipi nyumbani kwenu wekezeni pia mkumbuke kusaidia ndugu zenu, alisema.

Aidha amewasisitiza katika kuchangia maendeleo , kutafuta masoko ya bidhaa za hapa nyumbani kama vile matunda, kuchota ujuzi wa ughaibuni na kuuleta nchini kwani njia hii itachangia kuleta  maendeleo  ya nchi.

Wakati huohuo Kikwete amewaeleza DIASPORA kwamba walisahau kutoa maoni yao katika mchakato wa katiba mpya wa kuwa na uraia wa nchi mbili hivyo wakajikuta wakibaki katika siasa.

"Kilio na mwenyewe lakini ninyi mkasahau kulia katika kilio chenu cha kuwa na uraia pacha katika katiba mpya mkabaki mkitoa maoni juu ya mambo ya siasa mimi nawasoma katika blogs mbalimbali  lakini hamkukumbuka kutoa kilio chenu hivyo nawashauri labda muende bungeni kama wanavyofanya wakulima na wafugaji mkawaeleze wabunge wanaoendelea na bunge mjini Dodoma wawakumbuke katika kilio chenu" alisema Kikwete.
Kongamano hilo la  kwanza la DIASPORA lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda, Mkurugenzi wa DIASPORA Tanzania Emmanuel Mwachullah, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mwanaidi Maajar.

No comments:

Post a Comment