TANGAZO


Thursday, August 7, 2014

Pistorius:Mawakili watoa kauli ya mwisho

Oscar Pistorius amejitetea kwamba alimpiga risasi kimakosa mpenzi wake Reeva

Upande wa mashitaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mwanaridha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, imeanza kutoa kauli yake ya mwisho kuhusiana na kesi hiyo.
Hii ni kabla ya mahakama kutoa umauzi wake wa mwisho kuhusu hatma ya mwanariadha huyo.
Wakili wa upande wa mashitaka Gerrie Nel amesema sio ukweli kuwa Pistorius alimpiga risasi mpenzi wake kimakosa akidhani kwamba alikuwa jambazi.Bwana Pistorius anatuhumiwa kwa mauaji ya mpanzi wake, Reeva Steenkamp, nyumbani kwake mjini Pretoria mwaka jana.
Mauaji hayo yalitokea tarehe 14 mwezi Februari mwaka jana.

Kiongozi wa mashitaka Gerrie Nel
Wakili wa Pistorius pia anatarajiwa kutoa kauli yake ya mwisho kuhusiana na kesi hiyo.
Kesi hiyo iliahirishwa mwezi jana kablahatua hii ya pande zote kutoa kauli zao za mwisho kabla ya kesi kuamuliwa kufika.
Bwana Pistorius alisema alimpiga risasi Reeva kutokana na uoga kwani alidhani alikuwa mwizi aliyekuwa amevamia nyumba yake.
Hata hivyo wakili wa upinzani ameambia mahakama haipaswi kuwa a ugumu wowote katika kukataa ushahidi wa Pistorius kwa sababu hauna msingi na kwamba ni uongo.
Pia amesema Pistorius amejidai kuwa mwathiriwa kwa njia moja au nyingine kutokana na ulemavu wake.
Babake Pistorois ambaye hajakuwa maishan mwake kwa miaka mingi alikuwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kesi hiyo kuanza kusikilizwa. Babake marehemu Reeva pia alifika mahakamani kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment