*Alakiwa kifalme Simba
*Atamba kurudisha heshima Msimbazi
*Atamba kurudisha heshima Msimbazi
Kocha Patrick Phiri, akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, mara baada ya kuwasili nchini leo, kwa ajili ya kuifundisha timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.
Kocha Patrick Phiri, akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, mara baada ya kuwasili nchini leo, kwa ajili ya kuifundisha timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.
Kocha Patrick Phiri, akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, alipowasili nchini leo, kwa ajili ya kuifundisha timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.
Kocha Patrick Phiri, akielekea kwenye gari Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, alipowasili nchini leo, kwa ajili ya kuifundisha timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.
Kocha Patrick Phiri, akiwa uwanjani hapo, alipowasili nchini leo, kwa ajili ya kuifundisha timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.
Kocha Patrick Phiri, akielekezwa jambo alipowasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kuifundisha timu ya Simba.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri (wapili kulia), akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na baadhi ya viongozi wa Simba, mara baada ya kuwasili uwanjani hapo leo.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri (wapili kulia), akifurahia jambo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na baadhi ya viongozi wa Simba, mara baada ya kuwasili uwanjani hapo leo.
Kocha Patrick Phiri akiangalia mashabiki wa timu ya Simba, waliofika kumpokea uwanjani hapo leo.
Kocha Patrick Phiri, akisubiri kuondoka uwanjani hapo, mara baada ya kuwasili leo, akitokea nchini kwao, Zambia kwa ajili ya kuifundisha timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.
Kocha Phiri akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa Simba, mara baada ya kuwasili uwanjani hapo leo.
Wanachama na mashabiki wa timu ya Simba, waliofika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kumpokea Kocha wao mpya, Patrick Phiri, wakifurahia ujio huo, uwanjani hapo leo.
Wanachama na mashabiki wa timu ya Simba, waliofika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kumpokea Kocha wao mpya, Patrick Phiri, wakifurahia ujio huo uwanjani hapo leo.
Kocha Patrick Phiri, akiwasalimia wanachama na mashabiki wa timu hiyo, uwanjani hapo leo.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, akizungumza na waandishi wa habari, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo leo.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, akizungumza na waandishi wa habari.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, akivishwa shada la maua na mmoja wa wanachama wa Tawi la Mpira Pesa, Joyce Nangu, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, akivishwa shada la maua na mmoja wa wanachama wa Tawi la Mpira Pesa, Joyce Nangu, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, akikabidhiwa shada la mau na mwanachama Joyce Nangu wa tawi la Mpira Pesa.
Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam pamoja na baadhi ya wanachama na mashabiki wa timu ya Simba leo, uwanjani hapo.
Gari lililombeba Kocha mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri, likiwa limezungukwa wanachama pamoja na mashabiki uwanjani hapo.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
KOCHA mpya wa timu ya Simba, Patrick Phiri ametua nchini leo na kupokelewa na mamia ya mashabiki wa timu hiyo, huku akitamba atarudisha heshima iliyopotea kwa timu hiyo.
Phiri aliwahi kuifundisha Simba kuanzia mwaka 2003 na kuondoka 2005 kabla ya baadaye kurudishwa tena na kuipa ubingwa msimu wa 2004/2005 na msimu 2009/2010 alichaguliwa kuwa kocha bora wa msimu.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo, Phiri alisema anashukuru kupata nafasi nyingine ya kufundisha Simba kwani ni timu anayoijua vizuri.
"Niwashukuru viongozi wa kamati ya utendaji kwa kunipendekeza kuja tena kufundisha Simba, ninawaahidi mashabiki na wanachama wa Simba nitafanya kazi
kwa nguvu zangu ili kurudisha heshima iliyopotea," alisema Phiri.
Alisema licha ya kuwa nchini Zambia lakini alikuwa akiifuatilia kwa karibu na ndio maana anajua amekuja kwa kazi moja tu kuhakikisha timu hiyo inarudisha
heshima yake ya zamani.
"Tanzania ni kama nyumbani kwangu, kuna wakati nimepata maisha mazuri na pia mabaya hayakosekani lakini kikubwa ni lazima kuhakikisha ninaipa ubingwa
Simba nadhani hiyo ndio kiu ya muda mrefu ya mashabiki wa timu hii," alisema.
Phiri aliyekuwa mchezaji na pia kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo', alipokelewa kwa shangwe na nderemo huku mashabiki wa Simba wakipiga na kucheza ngoma kutokana na furaha ya ujio wa kocha huyo.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya timu hiyo, Collin Frisch aliyeongoza mapokezi ya kocha huyo alisema bado hawajafikiana ni mkataba wa muda gani atasaini lakini baada ya kuafikiana wataweka wazi.
"Kwakweli tumefanya mazungumzo ya awali tu na kuna baadhi ya vitu tumeshakubaliana ila kwakuwa ndio amefika tutampa muda wa kupumzika na kesho tutakaa naye tujue tutaafikiana vipi kuhusu mkataba tutakaoingia naye," alisema Frisch.
Kocha huyo atarithi mikoba iliyoachwa na Kocha Zdravko Logarusic 'Loga' alitimuliwa na uongozi wa Simba siku 19 baada ya kuingia naye mkataba wa mwaka mmoja, ikiwa ni siku moja baada ya kufungwa mabao 3-0 na Zesco katika mechi ya kirafiki ya Simba Day.
No comments:
Post a Comment