TANGAZO


Saturday, August 9, 2014

Nigeria yatenga fedha kukabili Ebola


hatua za kukabili ugonjwa wa Ebola
Rais wa Nigeria Goodluck Johnathan ametangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kama janga la kitaifa na kutenga zaidi ya dola millioni 11 kama mfuko wa kukabiliana na ugonjwa huo.
Shirika la Afya duniani WHO linakadiria kwamba takriban raia 960 wamefariki kutokana na ugonjwa huo nchini Guinea,Sierra Leone,Liberia na Nigeria.
Shirika la mafuta nchini Nigeria limefunga mojawapo ya kliniki zake kufuatia kisa kimoja cha ugonjwa huo.
Nacho kiwanda kikubwa cha kutengeza vyuma duniani ArcelorMittal kimeanza kuwaondoa wafanyikazi wake katika migodi yake ya chuma nchini Liberia kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment