TANGAZO


Monday, August 25, 2014

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta awatoa wasiwasi wasanii nchini kuhusu hakimiliki


Baadhi ya wasanii na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati walipohudhuria mkutano leo katika moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.

Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiwahutubia wasanii pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano leo katika kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia Suluhu Hassan akito maneno ya shukuurani kwa wasanii wakati walipofanya mkutano na Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta mkutano leo katika  moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia Suluhu Hassan akito maneno ya shukuurani kwa wasanii wakati walipofanya mkutano na Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta mkutano leo katika  moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.
Viongozi wa msafara walifuatana na wasanii 25 wakimsikiliza Makamamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia Suluhu Hassani wakati walipohudhuria mkutano leo katika moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazi wakati wa mkutano leo katika moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzani (TAF) Bw. Simon Mwakifamba (kushoto) akimkabidhi Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ripoti ya wasanii yenye mapendekezo mbalimbali kuhususiana na Katiba mpya wakati wa mkutano leo katika moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.

Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii walifika Bungeni mjini Dodoma kwa ajili kuwasilisha mapendekezo yao kwajili ya Katiba mpya. Kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma).


Na Benedict Liwenga, Dodoma.

MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sittaame watoa wasiwasi wasanii wa Tanzania wakati alipokutananao leo Bungeni mjini Dodoma kwalengo la kuwasikiliza wasanii haowakiwa na kilio chao cha kusahaulika kwa kipengele kinachohusu Haki Miliki (Intellectual Property) za kazi za wasanii katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Mhe. Sittaa mesema kuwa nidhahiriku wa Katiba iliyoposasa imepitwa na wakati kwani haigusii mambo mengine yakiwemo hakiya vitu visivyoshikika kama vile haki hizo za wasanii na wagunduzi hapa nchini.



“Tunachojaribu kufanya hapa Dodoma ni kutunga Katiba ambayo nirafiki kwa kila Mtanzania ili iweze kumsaidia kila mmojakatika eneo lake, hivyo hii itakuwa ni Katiba iliyorafiki”. Alisema Mhe. Sitta.

Aidha, Mhe. Sitta amewapongeza wasanii wote 25 waliowawakilisha wenzao kwakuja Bungeni mjini Dodoma kwaajili ya kuwasilisha mapendekezo yao iliyaweze kutambuliwa kwenye rasimu hiyo.



Wasanii hao ambao wamefuatana na viongozi wao wa msafara, pia amewapongeza kwa kazi kubwa na nzuri waifanyayo wasanii wengi wa Tanzania katika kuitangaza nchi yao.



Naye Mkuu wa msafara wa wasanii hao, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAF) Bw. Simon Mwakifwamba amemueleza Mhe. Sitta kuwa kuna umuhimu wa Katiba Mpya itakayopatikana ihakikishe inalinda Haki Miliki za wasanii pamoja na utambuzi wakundi kubwa la wasanii ndani ya Katiba hiyo kwani ndiyo wanafanyakazi kubwa ya kuitangaza Tanzania ndani na nje ya mipaka yake.



“Wasanii wanafanya kazi kubwa ya kuitangaza nchi ambapo kwasasa takwimu zamchango wao, katika Pato la Taifa kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2013 ya Chama cha Haki Miliki  cha Kimataifa kwa kipindi  cha mwaka 2007hadi mwaka 2010 sanaa zote imechangia kwa asilimia 4.3% zaidi ya madini, gesi, maji na hoteli, na tasnia ya sanaa imetoa ajira kubwa kwa zaidi ya asilimia 5.6%, hivyo naomba katika Katiba Mpya kuwepo nauungwaji mkono wa wasanii hasa katika kulinda Haki Miliki zao (Intellectual Property).



Kwaupande wake MakamuMwenyekiti wa Bunge hilo,Mhe. Samia Suluhu Hassan  aliwashukuru wasanii hao, kwa kufika Bungeni na kuja na jambo zuri lenye manufaa kwa wasanii na Taifa kwa ujumla na amewahakikishia kuwa maombi yao ya kutaka Katiba Mpya ilinde Haki Miliki za kazi zao ya tafanyiwa kazi.



“Kuja kwenu Dodoma katika shughuli hii kunaonyeesha jinsi mlivyo na upeo , hili ni jambo la msingi kuwekwa katika Rasimu ya Katiba. Huu ni wakati pekee wakuhakikisha mambo yenu yanatambulika,” alisemaMhe. Samia.



Aidha, Mhe. Samia aliongeza kuwa baada ya hapo kinachofuatia ni utungaji wa Sheria kupitia wizara husika.

No comments:

Post a Comment