Mchezaji mpira kutoka Cameroon amekufa baada ya kupigwa kichwani wakati mashabiki waliokereka waliporusha mawe mwisho wa mechi ya ligi ya Algeria.
Albert Ebosse, aliyekuwa na umri wa miaka 24, ndiye aliyetia magoli mengi kabisa katika ligi ya Algeria msimu uliopita.
Yeye ndiye aliyepata hilo goli moja kwa timu yake.Alirushiwa kitu wakati mashabiki walipokerwa kuwa timu yake, JS Kabylie, iliposhindwa kwa magoli mawili kwa moja katika mechi iliyochezwa nyumbani, Tizi Ouzou.
Wizara ya mambo ya nchi ya Algeria imeamrisha uchunguzi ufanywe.
Ligi ya Algeria imefunga uwanja wa mpira wa timu ya JS Kabylie na imeitisha mkutano wa dharura Jumatatu.
No comments:
Post a Comment