Msemaji wa chama tawala cha
Iraq kiitwacho Daawa, Dakta Zuhair Al Nahar, amesema kuna watu wengi
zaidi sasa wanaokubali kuwa Waziri Mkuu, Nouri al Maliki, anafaa
kuondoka madarakani:
"Kuna maoni kuwa Maliki, Waziri Mkuu Maliki, anafaa kumpisha mtu mwengine ambaye anaweza kuzileta pande zote pamoja.Maoni hayo yako hata ndani ya chama na kati ya washirika wengine wa waziri mkuu."
Dakta Zuhair Al Nahar alisema Iraq inahitaji kujibu sawa-sawa kijeshi na iwe na serikali yenye uwezo wa kuwashinda wapiganaji wa ISIS.
Waziri wa Mashauri ya nchi za nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ameisihi Iraq iunde serikali ya umoja itayojumuisha wengi ili kupambana na msukosuko huo.
Alisema hayo baada ya kuzungumza na mawaziri mjini Baghdad.
Na ndege za Marekani na Uingereza zimedondosha vifurushi vya chakula na mapipa ya maji kwa maelfu ya watu walionasa milimani baada ya kuwakimbia wapiganaji Waislamu wa kundi la ISIS kaskazini mwa Iraq.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani, (Rear Admiral John Kirby) alisema vifurushi vya chakula 50,000 na maelfu ya lita za maji, wamepatiwa wakimbizi wa madhehebu ya Yazidi walioko Mlima Sinjar.
Hii ni mara ya tatu kwa ndege za Marekani na mara ya kwanza kwa ndege za Uingereza kutoa huduma hiyo huko kaskazini mwa Iraq.
No comments:
Post a Comment