Liverpool imekubaliana na Sevilla ya Uhispania kumnunua Alberto Moreno kwa pauni milioni kumi na mbili (£12m).
Liverpool imethibitisha kuwa ilikubaliana na Sevilla, na itakamilisha mpango wa kumnunua Moreno siku chache zijazo.Alberto, 22, mwenye asili ya kispanyola anatarajiwa Merseyside kufanyiwa uchunguzi wa kiafya baadaye wiki hii.
Moreno alibubujikwa na machozi siku ya Jumanne baada ya Real Madrid kuibuka mshindi dhidi ya Sevilla kule Cardiff, huku akiaga mashabiki wa Sevilla, maafisa wa timu na wachezaji wenza.
Baada ya mchuano huo, meneja wa Sevilla, Unai Emery alisema: “Tuko Uingereza, karibu na timu zinazommezea mate Alberto.
Tunamtakia kila la kheri. Sasa itatubidi tutafute mchezaji mwingine atakayefana.”
Moreno na Jose Enrique sasa wanapigania nafasi ya kuwa beki wa timu ya Liverpool.
Enrique, 28, ambaye pia ana asili ya kispanyola alishiriki katika michuano tisa mwanzo wa msimu uliopita akishirikiana na Glen Johnson na Jon Flanagan.
Enrique hakushiriki hadi mwishoni mwa msimu kwani baadaye msimu huo alifanyiwa upasuaji kwa goti lake, Novemba mwaka uliopita.
Liverpool pia ilinunua wachezaji watatu kutoka Southampton Rickie Lambert, Adam Lallana na Dejan Lovren.
Aidha ilimnunua Lazar Markovic wa Benfica na Emre Can wa Bayer Leverkusen, huku Javier Manquillo wa Atletico Madrid akikopwa na kujiunga na timu hiyo kwa misimu miwili.
Martin Kelly anatarajiwa kuondoka Anfield na kujiunga na Crystal Palace.
Martin, 24, mwenye asili ya kiingereza, atarajiwa kufanyiwa upelelezi wa kiafya kwa kipindi cha masaa 24 na kujiunga na Crystal Palace.
Hapo awali klabu hizo mbili ziliafikiana kumnunua Kelly kwa pauni milioni moja nukta tano (£1.5m), lakini baadaye kuafikiana pauni milioni mbili (£2m).
No comments:
Post a Comment