Bunge la Libya
Bunge jipya la Libya limeshtumu muungano wa wanamgambo ambao unajaribu kuuteka uwanja wa ndege wa mji wa Tripoli.
Bunge hilo limeutaja muungano huo kuwa wa kigaidi na kuongezea kuwa vikosi vya taifa hilo vitakabiliana nao.
Muungano huo unashirikisha wanamgambo wa kiislamu pamoja na wanamgambo kutoka mji wa Misrata.
Msemaji wa wapiganaji hao amesema kuwa bunge hilo ni haramu na kutaka kurudishwa kwa baraza la kitaifa lililotawaliwa na waislamu.
Wanamgambo hao wanasema kuwa wameuteka uwanja wa ndege wa Tripoli lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa kwamba mapigano yanaendelea viungani mwa mji huo kati ya makundi pinzani ,huku milipuko ikisikika.
No comments:
Post a Comment