Shirika la kutetea haki za
binadamu Human Rights Watch limechapisha ushahidi wa kile linachokitaja
kuwa visa vya ukiukwaji wa haki za kibinadamu katIka maeneo
yanayoshikiliwa na waasi wa Ukraine wanaoiunga mkono Urusi.
Human Rights Watch lasema wapiganaji hao wa
waasi walioko majimbo yanayotaka kujitenga ya Donetsk na Luhansk
mashariki mwa Ukraine wamekuwa wakiwazuilia mamia ya raia ,wakiwemo
waandishi habari, wanaharakati na hata baadhi ya viongozi wa kidini
wanaounga mkono serikali ya Ukraine.Yeyote anaeonekana kuunga mkono Ukraine hudhalilishwa huku wengine wakiteswa kwa kupigwa , kuchomwa kwa sigara , kudungwa visu au kuteswa kisaikologia kwa vitisho kuwa watauawa.
Ripoti hiyo pia inasema ina ushahidi wa mauji ya kiholela kufanyika.
Mwandishi wa ripoti hiyo Tanya Lokshina, anasema mateso na mauaji hayo hufanywa kwa mpangilio fulani....
No comments:
Post a Comment