TANGAZO


Wednesday, August 27, 2014

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki limefunguliwa leo jijini Dar es Salaam

Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam, tangu utaratibu wa kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya. 
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Abdullah Juma Saadala (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Phyllis Kandie  (Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri kutoka Burundi), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo  Wilbert Kaahwa.
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika  Mashariki (EALA) wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge hilo Dkt. Margaret Zziwa (wa nne kutoka kulia waliokaa) na Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda, mara baada ya ufunguzi wa bunge hilo.
 Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Jumaa Saadala akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba ya Spika wa bunge hilo (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo

No comments:

Post a Comment