Kundi la wanamgambo wa Boko Haram limesema kuwa limebuni taifa la kiislamu katika miji na vitongoji inavyotawala kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau alizungumza kwenye kanda ya video iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji wake kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Gwoza mapema mwezi huu.
Jeshi la Nigeria limepuuza dai hilo kuwa “tupu.”Haijabainishwa iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii Muungano wa wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic State inayotawala sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq na Syria.
''ningependa kuwashukuru sana ndugu zetu ambao wamefanikiwa kukomboa ardhi na nyoyo za watu huko Iraq na Syria''
alisema bwana Shekau japo haikubainika iwapo ni wa moja au la.
''Nashukuru Allah kwa ndugu zetu waliokomboa mji wa Gwoza na wakaufanya kuwa sehemu ya himaya ya Islamic state," alisema bwana Shekau katika ukanda huo wa videowenye urefu wa dakika
Msemaji wa Jeshi la Nigeria Chris Olukolade alipinga tangazo hilo akisema kuwa ''hakuna hata nchi moja ya taifa hilo iliyotwaliwa na kuwa Nigeria ni moja. ''
Maelfu ya watu wameuwawa kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu 2009, wakati Boko Haram ilipoanza uasi wake.
Gwoza, iliyokuwa na wakazi 265,000 katika sensa iliyopita, ndiyo mji mkubwa zaidi ulio chini ya utawala wa Boko Haram.
Imepeperusha bendera zake juu ya Kasri ya Emir wa Gwoza, kiongozi wa kiasili wa mji huo, wakazi wanasema.
Boko Haram ni nani?
• Ilianzishwa 2002
• Hapo awali iliangazia kupinga elimu ya wazungu - Boko Haram inamaanisha " Elimu ya Magharibi ni haramu " kwa lugha ya Hausa
• Ilizindua operesheni za kijeshi 2009 ili kuunda taifa la kiislamu.
• Maelfu wauwawa, hususan kaskazini mashariki mwa Nigeria- lakini pia mashambulizi kwa polisi na makao makuu ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Abuja.
• Watu milioni tatu waathiriwa.
• Kutangazwa kuwa kundi la kigaidi na Marekani 2013.
Gwoza haiko mbali na Chibok, ambako Boko Haram iliteka nyara zaidi ya wanafunzi 200 wa kike mwezi Aprili.
Katika kanda ya video ya hapo awali, , bwana Shekau alipongeza taifa la kiislamu lakini hakuzungumza zaidi.
Maafisa wa polisi wa Nigeria wanasema wanatafuta askari 35 ambao hawajulikani waliko baada ya Boko Haram kushambulia shule ya polisi iliyoko Liman Kara, karibu na Gwoza wiki iliyopita.
Wakazi wanasema wanmgambo hao waliteka chuo hicho lakini haijabainishwa ni nani anayedhibiti chuo hicho.
Nigeria ilitangaza hali ya dharura katika majimbo matatu yaliyoko kaskazini mashariki mwa nchi 2013 lakini uasi uliendelea na hata kukithiri.
No comments:
Post a Comment