TANGAZO


Tuesday, August 12, 2014

Boko Haram: Wake wa Wanajeshi waandamana



Kundi la Boko Haram linatawala mji wa Gwoza

Wake wa wanajeshi wa Nigeria wameandamana Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wakipinga hatua ya jeshi kuwatuma waume wao vitani kukabiliana na wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram.
Maandamano hayo yaliyotokea nje ya kambi za jeshi zilizoko katika mji wa Maiduguri ilitokea baada ya serikali kutangaza kuwa inalenga kuukomboa mji wa Gwoza kutoka kwa wanamgambo hao.
Inakisiwa kuwa mamia ya raiya waliuawa juma lililopita wanamgambo wa Boko haram walipouteka mji huo wa Gwoza l kulingana na Seneta wa eneo hilo Ali Ndume.
Boko Haram imekuwa ikipigani kuunda jimbo linalojitawala kwa misingi ya Kiislamu kaskazini mwa Nigeria.


Baadhi ya Wanawake walioandamana
Mwandishi wa BBC aliyeko Abuja, Abdullahi Kaura Abubakar amesema zaidi ya wanawake 100 waliandamana katika kambi ya jeshi iliyoko Giwa karibu na mji wa Maiduguri, katika jimbo la Borno.
Kampeini ya Boko Haram ya kuwachinja wanajeshi ndiyo imewatia hofu kubwa familia ya wanajeshi hao .
Wanajeshi wa Nigeria wamekuwa wakilalamikia kuwa na vifaa duni na hivyo kushindwa na wapiganaji hao wa Boko Haram ambao wanatumia makombora na magari ya kisasa ya kivita .
Wanajeshi wa nigeria walimshambulia meja Generali Ahmed Mohammed, mnamo mwezi mei wakilmaumu kwa kuuawa kwa wenzao katika vita vilivyotokea katika kambi ya jeshi ya Maimalar .
Mwanamke mmoja aliyezungumza na BBC bila kusema jina lake anasema kuwa wanaume wao wamekuwa wakikabiliana na Boko Haram kwa miaka 6 sasa na kila walipouawa hakuna msaada waliopata kutoka kwa jeshi.


Kundi la Boko Haram linatawala mji wa Gwoza na sasa linaanza kufanya mashambulizi nje ya Nigeria
''Mwezi March waume wetu walishambulia Boko Haram siku iliyofwatia wapiganaji wa Boko Haram walivamia kambi yetu ambapo walichoma moto nyumba zetu na hakuna msaada tuliopata ''
''sasa hii leo wanataka kutuma waume wetu huko Gwoza ?
''Hatutakubali hilo kamwe !''
Wakaazi wa mji huo uliotekwa na kundi hilo wanasema kuwa miili ya watu ingali imetapakaa ovyo mabarabarani ikioza zaidi ya juma moja tangu Gwoza itwaliwe na kundi hilo.

No comments:

Post a Comment