Mataifa ya magharibi yametoa wito kwa Urusi kuyashinikiza makundi ya wapiganaji wanaounga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine kuhakikisha kuwa watu wanalifikia eneo la mkasa wa ndege ya Malaysia Airline ilioanguka siku ya Alhamisi.
Waziri mkuu nchini Uholanzi Mark Rutte amesema kwamba amemwambia rais wa Urusi Vladmir Putin,kwamba ana fursa ya mwisho kuonyesha kwamba anataka kusaidia.
Urusi imeyashtumu mataifa ya magharibi kwa kuzua habari za uvumi dhidi yake.
Urusi imesema kuwa maswali zaidi yanafaa kuulizwa kuhusu mfumo wa ulinzi wa anga ya Ukraine.
Hatma ya kisanduku cheusi kinacho rekodi yanayojiri katika ndege hiyo haijulikani huku viongozi wa waasi wakisema kuwa hakipatikani.
No comments:
Post a Comment