Aliyekuwa makamu wa Rais Nchini
Sudan Kusini, Daktari Riek Machar, anasema kuwa anachozungumzia kwa sasa
ni kutafuta sera ya mfumo mpya wa uongozi wa taifa hilo inayokabiliana
na mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Machar kwa sasa anaongoza vita vya upinzani
dhidi ya serikali ya Rais Kiir. Anasema kuwa anapigania mageuzi wala sio
kutaka wadhifa katika utawala wa sasa.Riek Machar ameiambia BBC kuwa mfumo huo unastahili kufaidi kila mtu Nchini humo na kuonyesha kuwa nchi hiyo ina demokrasia
Mwezi uliopita serikali na waasi walikubalina kuunda serikali ya umoja wa kitafa katika kipindi cha siku sitini.
Lakini baada ya kuulizwa ikiwa hilo litafanyika bwana Machar alikataa kujibu.
Sudan Kusini ilipata uhuru miaka mitatu iliyopita lakini mwaka uliopita ilitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
No comments:
Post a Comment