Serikali ya Nigeria inahitaji
msaada wa dola billioni moja ili kukabilina na wanamgambo ambao
wameliharibu taifa hilo katika miaka ya hivi karibuni.
Rais Goodluck Jonathan ametuma barua katika
bunge la seneti ili kuidhinisha ombi hilo ambalo litasaidia kuimarisha
vifaa vya kijeshi.Zaidi ya watu 2000 wameuawa mwaka huu katika ghasia zilizosababishwa na wapiganaji wa Boko haram.
Huku umwagikaji wa damu ukiendelea Kazkazini mwa Nigeria ,rais Goodluck Johanathan anaendelea kupata shinikizo.
Kuna ripoti kwamba wanajeshi wengi katika vita vya kukabiliana na wanamgambo hao hawana vifaa vya kutosha na hivyo basi kushindwa kuwakabili waasi hao.
Ijapokuwa jeshi halijakiri kuhusu madai hayo linakubali kwamba linahitaji vifaa zaidi ili kukabiliana na vita hivyo.
Rais Goodluck Johnathan anasema kuwa kuna umuhimu wa kulinunulia jeshi vifaa zaidi ili kukabiliana na tishio la Boko Haram.
Wakosoaji hatahivyo wamelishtumu jeshi kwa utumizi mbaya wa raslimali zilizopo.
No comments:
Post a Comment