Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisaini
kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam
(DMI), mara baaada ya kuwasili chuoni hapo kuangalia shughuli
mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho na kuongea na wafanyakazi wa Chuo
hicho, mwanzoni mwa wiki. Kulia kwake anaemtazama ni Kaimu Mkuu wa Chuo
hicho, Kapteni Yasin Songoro.
Mkufunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), akimpa maelezo
ya namna ambavyo wahandisi wanaofanya kazi ndani ya chumba cha injini
ndani ya Meli wanavyoendesha mitambo hiyo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya
Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, wakati alipotembea chuoni hapo mwanzoni
mwa wiki kuongea na wafanyakazi wa chuo hicho.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akimsikilza
Kapteni Jumanne Karume, alipokuwa akimpa maelezo ya namna nahodha
anavyoendesha Meli, wakati alipotembelea Chuo Cha Bahari Dar es
Salaam(DMI), mwanzoni mwa wiki. Kushoto kwa Dk Tizeba ni Makamu Mkuu wa
Chuo hicho, Kapteni Yasin Songoro.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba
(aliyeweka mikono mfukoni), akimsikiliza Kapteni Peter Mkunja wakati
akimpa maelezo ya namna vyombo vya kujiokoa vinavyotumika endapo meli
itazama ama kupata hitilafu yoyote, wakati Naibu Waziri huyo
alipotembelea Chuo hicho Mwanzoni mwa wiki.
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Kapteni
Yasin Songoro, akitoa maelezo ya namna ambavyo mashine inayotengeneza
vipuri vinayoharibika ndani ya meli inavyofanya kazi kwa Naibu Waziri wa
Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, alipotembelea Chuoni hapo
Mwanzoni mwa wiki hii.
Sehemu ya Menejimenti na wafanyakazi wa Chuo cha Bahari Dar es
Salaam (DMI), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk.
Charles Tizeba (Hayupo Pichani), wakati alipoongea nao mwanzoni mwa
wiki. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
No comments:
Post a Comment