Kikundi cha vijana toka Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala, wakisherehekea wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru uliokabidhiwa kwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Mwantumu Mahiza leo, Jijini Dar es Salaam.
Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani), akishiriki kucheza
pamoja na Kikundi cha vijana toka Manispaa hiyo,
wakati wa kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru leo, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, James Kajugusi (katikati), akiwaeleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi.
Sihaba Nkinga (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo, Prof. Elisante Ole
Gabriel wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru leo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi alipowasili wakati wa kuukabidhi mwenye wa uhuru kutoka wilaya.
Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana
na Vijana wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa walipowasili kutoka Wilaya ya Mafia
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo akikimbiza Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kuukabidhi tayari kuanza ziara yake Mkoani Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo (Mwenye T-shirt
nyeupe) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi.
Mwantumu Mahiza Leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza akikimbiza mwenge wa Uhuru Tayari kwa kuukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki.
Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Kiongozi wa mbio za
Mwenge Taifa, Rachel Kasanda wakati wa kuwasili kwa mwenge wa uhuru leo Jijini
Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza
akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki leo Jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa neno la
shukrani kwa Mkuu wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza kwa Kuukabidhi mwenge wa Uhuru
Salama Mkoani Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili mkoani Dar es Salaam.
Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili mkoani Dar es Salaam. (Picha zote na Hassan Silayo na Benjamin Sawe)
No comments:
Post a Comment