TANGAZO


Wednesday, July 23, 2014

Mlipuko waua 40, Nigeria


Watu wapata 40, wameuawa katika milipuko mikubwa miwili iliyotokea katika mji wa Kaduna, kaskazini mwa Nigeria. Katika mlipuko wa kwanza wa kujitoa mhanga watu 25 waliuawa, huku wengine 15 wakiuawa katika eneo lililokuwa na msongamano wa watu katika mji wa Kawo.
Shambulio hilo pia lilimlenga kiongozi wa upinzani na kiongozi wa zamani wa kijeshi Jenerali Muhammadu Buhari.
 
Shambulio la kwanza lilimlenga kiongozi mashuhuri wa kiislam aliyeambatana na wafuasi wake alipokuwa akitoka katika eneo la katikati ya Kaduna alikomaliza kufanya muhadhara kwa ajili ya mwezi mtukufu wa ramadhani. Maelfu ya watu walihudhuria tukio hilo la mwaka.
Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo, watu 25 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Shambulizi la pili lilimlenga kiongozi wa juu wa upinzani ambaye pia ni rais wa zamani Jenerali Muhammadu Buhari ambako nako wamekufa watu 19. Wote wawili, kiongozi wa kiislam na kiongozi wa upinzani wamenusurika bila kujeruhiwa.
Mwanahabari wa BBC amesema aliona viungo vya binadamu vikiwa vimetapakaa katika eneo kubwa la mlipuko. Kamishina wa polisi wa jimbo la Kaduna Alhaji Umar Usman Shehu amesema mlipuko ulisababishwa na anayehisiwa kujitoa muhanga.
Hakuna kundi lolote lililojitokeza kuhusika na mlipuko huo. Kundi la Boko Haram ambalo bado linawashikilia wanafunzi wasichana 200 kwa takribani siku 100 sasa, limeshafanya matukio ya kulipua mabomu kwa kujitoa muhanga katika miji mingi kaskazini mwa naijeria ukiwamo mji mkuu Abuja.

No comments:

Post a Comment