TANGAZO


Tuesday, July 22, 2014

Mchezaji mwingine mweusi abaguliwa


Seko Fofana, Manchester City
Mchezaji katika mashindano ya vijana wenye umri wa miaka 21 wa klabu ya Manchester amelazimika kutoka nje ya uwanja katika mchezo wa kirafiki kwa madai ya kufanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi.
Seko Fofana wa Manchester City Mfaransa mweusi mwenye umri wa miaka 19 aanadai kufanyiwa vitendo hivyo wakati timu yake ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Crotia, ambapo mmoja wa wachezaji wa timu hiyo walimbagua kwa misingi ya rangi.
Machester City imesema mchezaji huyo kiungo ndiye aliyelengwa na ubaguzi huo na mchezaji wa Croatia.
Hivi karibuni katika michuano ya kombe la Dunia shirikisho la soka ulimwenguni lilianza kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mashabiki wa timu ya Mexco ambao wanadaiwa kwua walifanya vitendo vya ubaguzi wa rangi.

No comments:

Post a Comment