Hali ya Tahadhari imetangazwa
mjini Freetown Sierra Leone baada ya mwanamke mmoja aliyeambukizwa Ebola
kutoroshwa kutoka Hospitalini na jamaa zake kwa hofu kuwa angekufia
huko.
Maafisa wa Usalama wa Umma na wale wa Afya
wanaendelea kumtafuta wakitumia vyombo vya habari na hata redio
kutangaza kuwa kuwepo kwake nje ya Hospitali na hatari kwa afya ya umma.Mama huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kudhibitishwa kuugua Ebola mjini Freetown.
Mwanume huyo ambaye ni raia wa Liberia, aliwasili Jumapili Lagos, kupitia Togo na mara akaanza kuugua na ugonjwa unaofananishwa na Ebola.
Mgonjwa huyo alikuwa ametengwa ilikufanyiwa uchunguzi kwani hakujakuwa na mgonjwa yeyote wa Ebola nchini Nigeria licha ya Ugonjwa huo kuenea kote katika mataifa ya magharibi mwa Afrika.
Iwapo itadhibitishwa kuwa alikuwa anaugua Ebola basi yeye ndiye atakayekuwa mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini humo.
Virusi vya ugonjwa huo husababisha uvujaji mwingi wa damu na katika zaidi ya nusu ya visa vilivyoripotiwa, waathiriwa wamefariki. Hakuna chanjo dhidi Ebola.
No comments:
Post a Comment