TANGAZO


Saturday, July 19, 2014

Kundi la Alshabaab lashambulia tena Lamu



Shambulizi la Alshabaab nchini kenya
Kundi la Alshabaab limekiri kutekeleza shambulizi katika basi moja la abiria katika pwani ya Kenya hapo jana usiku.
Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu saba walipigwa risasi na kufariki huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Watu kadhaa wameuawa katika Pwani ya Kenya katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita.Shambulizi hilo lilitokea katika mji wa Witu katika Kaunty ya Lamu.
Kundi la Alshabaab limekiri kutekeleza mauaji hayo.
Linasema kuwa linalipiza kisasi kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini Somali.
Ghasia hizo zimeathiri pakubwa sekta ya utalii nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment