Kulia Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Suleiman Nkamia akipeana mkono na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa Group Said Muhammad Said Abeid mara baada ya kumkabithi Hundi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 93,000 kutoka kwa Kampuni ya Bakhresa Group kwa ajili ya kusaidi timu za wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola jijini Glasgow Scotland.Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari leo jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Suleiman Nkami, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, Meneja Chapa wa Kampuni ya Bakhresa Group, Katibu wa Naibu Waziri Bw. Francis Songoro na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa Bw.Said Muhammad Said Abeid wakifurahia mara baada ya makabidhiano ya hudi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 93,000/= ikiwa ni msaada wa kampuni hiyo kwa wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Scotland.
Baadhi ya waandishi wa habari wakishuhudia makabidhiano ya
hundi ya mfano kutoka kwa wawakilishi wa Bakhresa Group katika hafla
iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
leo jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo imetoa msaada wa Dola za Kimarekani
93,000 ili kusaidia timu za wanamichezo wanaoshiriki Mashindano ya Jumuiya ya
Madola yanayotaraji kuanza rasmi tarehe 23 mwezi huu huko mjini Glasgow
Scotland.
Na Rose Masaka-MAELEZO
NAIBU wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Juma Nkamia amemuomba mmiliki wa kiwanja cha michezo cha Azam Complex Bw. Said Salim Bakhresa kutoa ruhusa kwa wachezaji wa Tanzania kufanya mazoezi katika uwanja huo hasa wakati wa usiku ili ziweze kuwa katika nafasi nzuri na zipate uzoefu wa kucheza muda huo.
Hayo yamesemwa leo, na Mhe. Nkamia katika kikao cha kukabidhiwa cheki na Bw. Bakhresa yenye thamani ya Dola 93,000 ili kuisaidia timu ya Taifa ya riadha kufika Glasgow, Scotland pamoja na mahitaji mengine kama jezi na vifaa.
“Fedha hii itasaidia timu yetu yenye wachezaji 39 ,makocha, pamoja na walimu waliotoka China kuweza kurudi salama.” Alisema Nkamia.
Aidha, Mhe. Nkamia ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuweza kuzungumza na wachezaji hao na kuwakabidhi bendera ya Taifa huko waendako.
Bw. Bakhresa amesema kuwa anaisapoti timu ya Taifa kwenda Scotland kwa sababu michezo siyo mpira wa miguu tu na amefafanua kuwa mashindano ya michezo ni kitu muhimu katika nchi na kinaleta maendeleo.
“Tunachokipata kinatokana na jasho la watanzania na tunakirudisha kwa watanzania,Tanzania inajengwa na watanzania wenyewe siyo watu wa nje”. Alisema Bakhresa.
No comments:
Post a Comment