Kumetokea ufyatulianaji mkali wa risasi katika kambi ya kijeshi
katika mji mkuu wa Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa zinasema kuwa raia wameondolewa katika eneo hilo na haijafahamika
makabiliano hayo yaliyotokea katika kambi ya wanajeshi wa kumlinda rais
yametokana na nini.Taarifa kutoka kwa serikali zinasema kuwa wavamizi walijaribu kupenyeza katika kambi ya kijeshi ya Camp Tshatshi na makabiliano yalizuka kwa zaidi ya dakika 30 hivi.
Jamhuri hiyo ya Kidemokrasia ya Congo imesakamwa na vita kwa kipindi kirefu sasa na hata rais aliyepo madarakani kwa sasa Joseph Kabila alichukua mamlaka baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka wa , 2001.
Raiya walihamishwa kutoka maeneo yaliyoko karibu na uwanja wa ndege ulifungwa wakati wa shambulizi hilo.
Serikali bado haijamtaja nani aliyeishambulia .
Hii sio mara ya kwanza kwa Camp Tshatshi kushambuliwa mwaka uliyopita kami hiyo ilishambuliwa tena na wakati huo wafuasi wa dini ya ya kikristo ya dhehebu linaloongozwa na Paul Joseph Mukungubila walilaumiwa.
No comments:
Post a Comment