Israeli imeendelea kuivirumishia
makombora Gaza kucha kutwa ,huku kikao cha mawaziri wa baraza la
Usalama kikitarajiwa huko Marekani kujadili mapendekezo mapya ya wito
wa kusitishwa mapigano kwa misingi ya kibinadamu.
Afisa wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa
aliyeko Gaza Bob Turner, ameiambia BBC kuwa wapalestina laki moja unusu ,
ambao ni asilimia 8 ya idadi ya watu wa Gaza sasa wamekimbilia hifadhi
kwenye shule za Umoja wa mataifa.Idadi ya raia wa Palestina waliouawa imezidi mia nane, huku mashambulio hayo ya Israel ya angani majini na ardhini yakiingia siku ya kumi na nane.
Wanajeshi 32 na raia watatu wa Israel wameuawa katika muda huo.
Katika ukingo wa magharibi, na Jerusalem mashariki raia wawili wa Palestina wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati waandamanaji waliokuwa na hasira kuhusu mashambulio huko Gaza walipokabiliana na vikosi vya Israel.
Hata hivyo Bwana Moon na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry wanaendeleza juhudi za kutafuta makubaliano ya kusitisha vita.
Kerry alikuwa Cairo kukutana na waziri wa maswala ya kigeni wa Misri Sameh Shoukry na Ban Ki-moon ambapo wanajaribu kuishinikiza Hamas kukubali mwito wa kusitisha mapigano bila ya kuishinikiza Isareli kuondoa vikosi vyake katika ukanda wa Gaza.
Mapema leo maandamano makubwa yalifanyika katika ukingo wa Magharibi mwa Palestina karibu na mpaka wake na Israel kupinga mashambulio yanayofanywa na Israel.
Waandamanaji hao wakiwa na hasira walipambana na vikosi vya usalama vya Israel.
Hata hivyo mapambano makubwa dhidi ya vikosi vya usalama ilikuwa katika eneo la Qalandia katika mpaka wa Ramallah and Jerusalem.
No comments:
Post a Comment