Mjumbe maalumu wa Umoja wa
Mataifa nchini Iraq amewaambia wanasiasa wasonge mbele kuunda serikali
ama sivyo kuna hatari ya nchi kuingia kwenye mtafaruku.
Katika taarifa yake, Nickolay Mladenov, alisema
Iraq ikishindwa kuteua watu kushika nyadhifa tatu - rais, waziri mkuu na
spika - basi itasaidia masilahi ya wale wanaotaka kuigawa Iraq.Mataifa makuu yamewasihi wanasiasa wa Iraq waungane kupambana na kundi la ISIS, ambalo limeteka maeneo makubwa ya nchi.
Bunge la Iraq linatarajiwa kukutana Jumapili.
Kikao cha bunge cha tarehe mosi Julai kilimalizika kwa chuki na wabunge wa Sunni na Kurd walitoka nje.
No comments:
Post a Comment