TANGAZO


Sunday, July 13, 2014

Fainali: Argentina vs Ujerumani


Wachezaji wanaotarajiwa kufunga mabao katika fainali

Jumapili ya tarehe 13 Julai mwaka wa 2014 hatimaye imewadia .
Macho yote duniani yatakuwa yanaelekea katika uwanja wa Maracana ulioko Rio Brazil ambapo mechi ya fainali ya kombe la dunia itakuwa ikichezwa.
Mahasaimu wa Jadi Argentina watakuwa wakichuana na Ujerumani katika fainali yao ya tatu katika historia ya kombe la dunia.
Mechi hiyo ndiyo itakayokuwa kilele cha majuma manne ya kipute hicho kilichojumisha timu 32 kutoka mabara yote 5 zikichuana miongoni mwao katika miji 12 ya Brazil kuanzia juni tarehe 12 .
Hayo yote ni kenda timu hizo zote zilikuwa zikiwania kuandikisha majina yao kwenye tuzo la kipekee la dhahabu yaani kombe la dunia.
Katika mechi hii ya leo Mahasimu hawa wanafahamiana sana.


Mashabiki wakijiandaa kwa fainali ya kombe la Dunia
tayari wamechuana mara saba tatu zikiwa ni katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 1986 na 1990.
Ujerumani ilishinda mara moja nayo Argentina ikaibuka mshindi mara moja kwa hivyo hii leo itakuwa mechi ya kukata na shoka .
Wajermani wakiandikisha rekodi kwa kuinyeshea wenyeji Brazil jumla ya mabao 7-1 katika nusu fainali huku Argentina nayo ikihitaji muda wa ziada na hata mikwaju ya penalti kuibandua Uholanzi na kufuzu.
Ujerumani itakuwa timu ya kwanza kutoka bara Ulaya kutwaa kombe la dunia katika Marekani ya kusini iwapo itaipiku Argentina.


Timu ya Argentina itakayochuana na Ujerumani katika fainali ya kombe la duniahuko Brazil.
Argentina nayo inakumbuka vyema matukio ya miaka 28 iliyopita ilipoilaza Ujerumani Magharibi wakati huo na kutwaa kombe lao la mwisho la dunia je Historia itajirudia ?
Kama ilivyokuwa katika mech za awali Argentina itakuwa inamtegemea Lionel messi kwa ufungaji mabao kwani hata sasa Di maria bado ni shaka iwapo atacheza au la kutokana na jeraha la paja.
Iwapo atafaulu katika Fainali ,Messi atakuwa bila shaka katika mizani sawa na aliyekuwa nyota wa Argentina Diego Maradona na hata kumpiku kocha huyo wa zamani.
Kwa Upande wao Ujerumani imesifiwa kwa kuwa na uwezo wa kipekee wa kucheza kama kikosi wala sio kumtegemea nyota mmoja kwa ufungaji mabao.


Timu ya Ujerumani itakayochuana na Argentina katika fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Vijana wa Joachim Loew wanamtarajia mfungaji wao nyota Miroslav Klose akisaidiana na Thomas Muller kuwapa mabao na hatimaye ushindi dhidi ya Argentina .
Takriban tiketi elfu 75.000. zimeuzwa na hadi sasa kinachosubiriwa ni kujua iwapo mashabiki wa Brazil watawashabikia majirani wao lakini hasimu wa jadi Argentina, ama timu iliyoandikisha rekodi ya kuifunga Brazil mabao mengi zaidi katika historia Ujerumani.
Dakika tisini zijazo ndizo zitakazoamua mbivu na mbichi .

No comments:

Post a Comment