*Wasailiwa 1,281 kuingia duru la mwisho ya usaili
WASAILIWA 1,281 kati
ya 6,115 waliofanya usaili wa kwanza tarehe 13 Juni, 2014 jijini Dar es Salam
kuomba nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji (Assistant Inspector of
Immigration) wanatarajiwa kuingia duru ya pili na ya mwisho ya usaili huo baada
ya kufanikiwa kufaulu usaili wa kwanza.
Usaili huu ambao
utafanyika kwa awamu utaanza tarehe 23 Juni hadi 03 Julai, 2014 na utafanyikia
katika Bwalo la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1.30
asubuhi.
Tofauti na usaili wa
kwanza ambao ulikuwa wa kuandika na ulihusisha maswali ya hesabu na ufahamu wa
jumla, usaili wa awamu ya pili utakuwa wa maswali ya ana kwa ana ambao
utahusisha kupima uwezo wa msailiwa kujieleza na kufafanua mambo.
Kuchaguliwa kwa
wasailiwa hawa kulifanyika baada ya kusahihisha majibu yao na majina kuingizwa
katika mfumo wa kimtandao ambao ulisaidia kuchagua wasailiwa waliopata alama
hamsini na kuendelea.
Majina ya wasailiwa
hawa yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, www.moha.go.tz
na ya Idara ya Uhamiaji, www.uhamiaji.go.tz
na watatakiwa kuja na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa, vya shule na picha mbili
za pasipoti.
Awali, kiasi cha wasailiwa 10,801 waliitwa kwa ajili ya
usaili wa kwanza baada ya kupokea maombi yao, lakini waliohudhuria ni 6,115 na
kati yao ndio walipatikana 1,281 ambao watasailiwa ili kupata watakaojaza
nafasi sabini (70) za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji katika Idara ya Uhamiaji.
Sgn
Isaac J. Nantanga
0754 484286
MSEMAJI,
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
18
Juni, 2013
No comments:
Post a Comment