Polisi nchini Kenya wamesema
kuwa wamewakamata washukiwa wawili wa mashambulizi yaliyofanyika mjini
Mpeketoni, Pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 60.
Kundi la wapiganaji wa Al Shabaab limekiri
kufanya mashambulizi hayo yaliyofanyika Jumapili usiki na Jumatatu usiku
ingawa serikali ya Kenya imesema kuwa mashambulizi hayo yalichochewa
kisiasa.Licha ya madai ya haraka kutoka kwa kundi la Al Shabaab kuwa wao ndio waliotekeleza mashmabulizi hayo, Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba yake kwa taifa alilaumu vikundi vya wanasiasa pamoja na makundi ya watu ambayo yana nia ya kufaidi kutokana na hali mbaya ya usalama nchini humo kwa kufanya mashambulizi hayo.
Maafisa kadhaa wa polisi wa eneo la Mpeketoni, wamefutwa kazi na wengine kuhamishwa kutoka vituo vyao vya kazi katika eneo hilo.
Hii ni baada ya tuhuma dhidi yao kuwa walipuuza onyo la kutokea kwa mashambulizi hayo kutoka kwa shirika la ujasusi. Wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka.
No comments:
Post a Comment