TANGAZO


Sunday, June 1, 2014

Wanajeshi washika doria mjini Bangkok

Wanajeshi walinda baadhi ya ofisi za serikali mjini Bangkok
Maelfu ya polisi pamoja na wanajeshi wamepelekwa katika mji mkuu wa Thailand Bangkok kwa jaribio la kuangamiza maandamano dhidi ya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi jana.
Baadhi ya vituo vya treni pamoja na maduka ya jumla yamefungwa kutokana na maandamano hayo.
Mwandishi wa BBC mjini Bangkok amesema kuwa eneo la biashara katikati ya mji huo limesalia kuwa mahame baada ya jeshi kulifunga.
Siku ya ijumaa kiongozi wa jeshi Jenerali Prayuth Chan Ocha aliziambia pande pinzani kushirikiana na kuwacha maandamano ili kuleta maridhiano.
Katika hotuba hiyo kiongozi huyo amesema kuwa uchaguzi mpya hautaitishwa hadi baada ya mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment