mwanajeshi wa Isis
Ripoti kutoka Iraq zinaarifu
kuwa vikosi vya serikali vilivyojaribu kuuteka mji wa Tikrit kutoka kwa
wapiganaji wa kisunni vimelazimika kurejea nyuma.
Walioshuhudia wanasema kuwa wanajeshi hao
walilazimika kurudi katika mji wa Dijla ,yapata kilomita 25 kusini baada
ya mashambulizi yao yalioshirikisha mizinga,magari ya kujihami na ndege
kushindwa kufua dafu.Hatahivyo kuna ripoti ya majeruhi wengi kutoka pande zote mbili.
Duru zimearifu kuwa vikosi hivyo vya serikali vinajitahidi kufika Tikrit kwa kuwa wapiganaji wa ISIS wametega vilipuzi vingi katika barabara kuu ya kuingia mjini humo.
Wakati huohuo Iraq inasema kuwa imepokea kundi la kwanza la ndege za kijeshi ilizoagiza kutoka Urusi ili kuisadia kukabiiana na wapiganaji wa dhehenu la kisunni ISIS ambao wameyateka maeneo mengi ya taifa hilo.
No comments:
Post a Comment