Uchunguzi unaohusisha vitengo
vitatu vya serikali ya Kenya umeanzishwa kufuatia madai ya mtoro wa
ugaidi anayesakwa duniani Samantha Lewthwaite, maarufu kama 'White
Widow' , anayedaiwa kuonekana katika eneo la Lamu pwani ya Kenya.
Maafisa wa uchunguzi wa jeshi la Kenya kwa
ushirikiano na maafisa wengine kutoka idara ya polisi na wizara ya
usalama wa ndani wanachunguza madai kuwa maafisa wa polisi mjini Lamu
walimpa ulinzi mama mmoja mzungu, ambaye alitoweka baada ya maafisa wa
forodha na uhamiaji kumzuia kuondoka Kenya na kuingia nchini Somalia.Ripoti zinasema kuwa polisi walimpa ulinzi mama huyo aliyedai kufanya kazi na shirika moja la kimataifa na alitaka kutembelea kambi ya wanajeshi wa Kenya nchini Somalia.
Alipofika eneo la mpakani la Kiunga maafisa wa uhamiaji walihoji uhalali wa stakabadhi zake na hivyo kumzuia kuondoka.
Mara tu baada ya tukio hilo, mama huyo alitoweka hadi sasa hajulikani aliko.
Msemaji wa majeshi ya Kenya, Willy Wesonga amethibitisha kuwa kundi la majasusi wamekabidhiwa jukumu la kuchunguza ikiwa kweli mwanamke huyo ni Samantha Lewthwaite na ikiwa ndiye, ni kwa nini alitaka kuzuru kambi ya wanajeshi wa Kenya.
Kamanda wa polisi katika kaunti ya Lamu, Leonard Omollo, amethibitisha kuwa maafisa wake walimpa ulinzi mama mmoja mzungu. Amesema wao hawakuwa na wasi wasi kwa kuwa aliwapa stakabadhi za kujitambulisha ila wao hawakuwa na hofu kuwa ni gushi.
Polisi pia wanalitafuta gari ambalo alikuwa amelikodisha baada ya kuthibitisha kuwa gari lilo hilo ndilo lililotumika majuma mawili yaliyopita katika shambulio dhidi ya wanajeshi wa Kenya ambapo wawili waliuawa na wengine kujeruhiwa.
Samantha aliwahhi kudaiwa kuhusina na mashambuliai ya kigaidi yaliyokumba jengo al kifahari la Kenya Westgate mwaka jana.
No comments:
Post a Comment