TANGAZO


Thursday, June 19, 2014

Ugonjwa wa kusahau umetelekezwa


Ugonjwa wa akili haupewi kipaumbele
Mtaalamu mashuhuri wa maradhi ya Ki-akili ya dementia ambayo huathiri uwezo wa kufikiri, Daktari Dennis Gillings, amejitokeza na kuzungumzia kile anachokiita, mwendo wa Kobe katika taratibu ya kupata tiba mpya ya ugonjwa huo. Ugonjwa huo wa akili unawaathiri zaidi ya watu milioni 4 kote Duniani.
Daktari Gillings ambaye aliteuliwa na waziri mkuu wa Uingereza mwaka jana amesema ahadi zilizotolewa na mataifa manene yenye uchumi mkubwa duniani G8 kutafuta tiba ya ugonjwa huo kufikia mwaka 2025 haziwezi kutimizwa bila kuwekeza zaidi katika utafiti.
Miezi sita baada ya ahadi hizo kutolewa wataalam kutoka maeneo mbalimbali duniani wanakutana London ili kujadili hatua zinazohitajika kuimarisha utafiti na majaribio ya dawa za kutibu ugonjwa huo.
Daktari Gillings anasema majaribio ya dawa hizi yanapaswa kudhibitiwa kuambatana na utaratibu wa majaribio ya dawa zingine.
Serikali ya Uingereza inatarajiwa kuwasilisha ripoti kuhusu ugonjwa huo nchini humo ambapo watu laki nane wameathirika. Wanasayasi pia watatoa ripoti itakayoangazia uhusiano wa Ugonjwa wa dementia na lishe.

No comments:

Post a Comment