TANGAZO


Wednesday, June 25, 2014

Ripoti yasema wanajeshi wa DRC waliuawa




Wanajeshi wa DRC Congo
Ripoti ya uchunguzi uliofanywa na madaktari wa Congo kuhusu vifo vya wanajeshi wake kufuatia vita vya mpakani kati ya Rwanda na wanajeshi hao inaonyesha kwamba huenda waliuawa.
Miili yao ilikabidhiwa DRC Congo na Rwanda siku kumi zilizopita kufuatia vita hivyo vya mpakani.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Rwanda Louis Mushikiwabo amesema kuwa wanajeshi hao waliuawa na wanajeshi wa Rwanda wakati wa vita baada ya kuingia katika ardhi ya Rwanda na kuwashambulia wanajeshi wake.
Ripoti hiyo ya mauaji ilibaini kuwa wanajeshi wote watano walikuwa na majeraha katika vichwa vyao,ikiwemo kifuani na tumboni huku dharubu ya majeraha hayo yakionekana kutekelezwa karibu.
Mmoja ya wanajeshi hao alionekana kupigwa risasi mara nane kutoka nyuma.


Wanajeshi wa DR Congo
Duru kutoka jeshi la Congo mjini Goma zimeambia BBC kwamba si rahisi kwamba watu hao walipata majeraha hayo wakati wa vita na kwamba huenda waliuawa kinyama.
Mapema juma hili BBC ilifanikiwa kupata ripoti kuhusu kisa hicho kutoka kwa wataalam wa kimataifa wa eneo la maziwa makuu waliopewa jukumu la kuchunguza yanayoendelea katika mpaka wa mataifa hayo mawili.
Rwanda ilidinda kutia sahihi ripoti hiyo.
Nakala hiyo inasema kuwa maeneo mawili ambayo Rwanda inadai kwamba wanajeshi hao wa Congo waliuawa wakati wa vita hayakuwa na mabaki ya risasi.
Ripoti hiyo pia inaonyesha ramani ya nchi hizo mbili katika eneo la Kanyesheja 2,ambapo inadai kwamba mlima unaopiganiwa na nchi hizo mbili uko ndani ya DR Congo.
Majeshi ya Rwanda yamejibu ripoti hiyo yakisema kuwa ramani ya Google sio thibitisho la ukataji wa mipaka.

No comments:

Post a Comment