TANGAZO


Friday, June 27, 2014

Raia wa Algeria washerehekea kufuzu



Raia wa Algeria washerehekea timu yao kufuzu kwa raundi ya pili.

Makumi ya maelfu ya mashabiki walishiriki katika sherehe nchini Algeria baada ya timu yao kufuzu kwa michuano ya mchujo ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.
Algeria ilifuzu katika awamu hiyo ya pili nchini Brazil baada ya kupata sara ya bao moja kwa moja na Urusi ambao waliobanduliwa katika michuano hiyo.
Fataki ziliwashwa usiku kucha katika mji mkuu wa Algeria, Algiers huku makundi ya raia wakicheza densi na kupeperusha bendera.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa sherehe hizo ziliendelea hadi asubuhi huku familia pia zikishiriki.
Misafara ya magari ilipitia katika maeneo mengi ya mji huo mkuu huku barabara tofauti zikigeuzwa na kuwa sehemu za kucheza densi.
katika miji mingi nchini Ufaransa idadi kubwa ya raia wa Algeria ambao ni mashabiki wa timu hiyo ya soka pia walijaa katika barabara za nchi hiyo wakisherehekea ushindi huo.
Katika raundi ya pili, timu ya Algeria itakabana koo na Ujerumani siku ya jumatatu.
Katika michuano ya dimba la dunia mnamo mwaka 1982,Ujerumani Magharibi ilishtumiwa kwa kucheza sare na Austria kimakusudi ili kuhakikisha kuwa timu zote mbili zinafuzu ili kuiondoa Algeria.

No comments:

Post a Comment