Miss Pwani wakiwa katika picha ya pamoja
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa Maisha Plus (Police Mess) kutafanyika tukio la aina yake la kumsaka Redds Miss Pwani 2014 usiku wa leo.
Katika Shindano hilo ambalo litakuwa ndiyo sehemu ya kuuzinduz ukumbi huo ambao leo hii ndiko kutakuwa na burudani kubwa ya muziki wa dansi kutoka katika bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Next level’ wakiongozwa na mzawa wa mkoa wa Pwani Ally Choki almaarufu kama ‘Mwarabu wa Kibaha’ ambao nao wameahidi kutoa burudani ya kihistoria kwenye onyesho hilo.
Bendi hiyo ambayo inatamba na vibao vingi ambvavyo vimeipa sika kama ‘Regina’ na nyinginezo (Zitaje)
Mbali ya Choki ambaye atakuwa na kikosi chake kikali cha wacheza shoo kinachoongozwa na Mussa Hassan Nyamwela pamoja na wanenguaji wa kike kama Maria Soloma , Asha Said ‘Sharapova’, Otilia na wengineo watanogesha na kuacha historia siku hiyo .
Katika shindano hilo jumla ya warembo Kumi watapanda jukwaani ambao Khadija Sihaba, Glory Jige, Irene Rajab, Mary Samwel, Arafa Shabani, Jeniffer David, Judea Joseph, Mary Mpelo,Roksana Msangi na Faith.
Mshindi wa Miss Pwani ndiye atapata nafasi ya kuuwakilisha Mkoa huo katika shindano la kanda ya Mashariki na baadaye katika fainali za Redd’s Miss Tanzania 2014.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii Mkurugenzi wa Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) ambaye pia ni mratibu wa shindano hilo Khadija Kalili alisema kwamba kila kitu kiko tayari hivyo ni wakati wa wakazi wa mkoa wa pwani n kujitokeza kwa wingi usiku wa leo (Ijumaa) kuja kumshuhudia mwakilishi wa mkoa wao yaani Redds Miss Pwani 2014.
Kalili aliongeza kwa kusema kuwa anawaahidi wakazi wa mkoa wa Pwani na wilaya zake zote kwa jumla kupata burudani ya aina yake siku hiyo hiyo ni kutokana kwamba Kampuni ya Linda kuanza vema kwa kuandaa mashindano yenye mvuto huku akitolea mfano wa ilivyokuwa katika shindano la Wilaya ya Kibaha mjini Redd’s Miss Kibaha 2013.
Kalili anasema anatoa shukrani zake za dhati kwa wadhamini wa shindano ambao ni wadhamini wakuu Redd’s Premium Cold, DIRA Media Group, Times FM, Radio5, Cloudes FM, Eden Herbalist Clinic ya Jijini Dar es Salaam, CXC Africa, Kitwe Traders, Michuzi Media Group, Jambo Concept, Bongoweekend.blogspot.com, Maisha Plus (Police Mess) , Montage.Kiingilio ni sh. 10,000.
No comments:
Post a Comment